Na nyie mmezidi ,muda mwingine tukiwamwaga
msiwe mnatulaumu kwani ni uzembe wenu
ndiyo unatusababisha.
Angalia, unajua kabisa Mimi ni Mume wa Mtu na nilishakueleza
kila kitu na hadi kukupa mwongozo mzuri tu wa jinsi Mimi na Wewe tutakavyokuwa
tunatenda " dhambi " zetu lakini bado hamsikii.
Nimekuambia:
1. Usinipigie Simu hadi Mimi nikupigie Wewe kwa makusudi
kabisa unanipigia usiku Saa mbili na hata Saa 6 au Saa 8 usiku.
2. Tukionana barabarani kama nikiwa na Mke wangu badilisha
njia au kama ni ghafla usinisalimu Wewe ukiniona tu na Mke wangu unanisalimu
kwa " mashamsham " ya Kimahaba kabisa.
3. Ukimjua au kuonana na Mke wangu kama umeshamjua basi mpe
heshima yake lakini Wewe ukionana na Mke wangu ndiyo unaanza " kumbinulia
" domo lako utadhani Ndege aina ya kinega anataka kujisaidia.
Enyi Michepuko! kama mmekubaliana na sheria za mchezo basi
jitahidi muwe mnazifuata kwani mmeshatukosesha wengine sasa Wake na sasa "
kimenuka " huku. Mnataka tuwapendeje? Mnaturoga tunawavumilia na
tunawapeni pesa za kutosha hamridhiki je tuwafanyeje?
Leo mmenipandisha kweli hasira na mlivyo na roho mbaya
umeshaona " umelikoroga " kwa Mke wangu sasa unataka uhamie kwangu leo
leo,Heh wee vepeeeee?.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni