Ukiona umemtumia mpenzi wako,mchumba
wako,mchepuko wako au hata rafiki wa kike wakati mwingine SMS ya kawaida tu
kwaajili ya kumsalimia lakini yeye akakujibu moja kati ya majibu yafuatayo,
tafadhali sana usiendelee kuchat nae maana kinachofuata hapo ni majanga tu.
Kwa mfano:
1. Ukimtumia sms ''Mambo mpenzi wangu?'' akikujibu ''mambo
mabaya'', usimuulize kwanini mambo mabaya, ukimuuliza atakwambia kuwa ''sina
hela dear''
2. Ukimtumia sms ''Maisha yanasemaje love?'' akikujibu
''maisha magumu hubby wangu we acha tu'' usimuulize kwanini, ukimuuliza kwanini
atakwambia ''nimefulia mwenzio kama nini sijui''
3. Ukimtumia sms ''Mbona kimya sana honie, umenitupa kiasi
hicho'' akikujibu ''sijakutupa wangu yaani mambo hata hayaendi'' usimuulize kwanini
mambo hayaendi, ukimuuliza atakwambia kuwa ''yaani sina kitu honie wangu, simu
ilikuwa haina hata hela ya kubeep''
4. Au ukiona mwanamke anaanza kwa kukwambia nikwambie kitu?
We mkatalie kiutani utani tu, mwambie usiniambie, hata akikomaa vipi akwambie
mwambie sitaki uniambie huku unafanya kama utani lakini moyoni unakuwa upo
serious.
Ni mara chache sana mwanamke akikwambia kuwa mambo mabaya,
maisha magumu au mambo hayaendi huwa na matatizo mengine kama kuumwa,
misiba.... n.k lakini THE REST ni wapigaji mizinga tu. Akikwambia maisha magumu
mjibu ''pole baby, mambo mengine vipi?''
Ukipewa majibu kama hayo, chagua moja, either usiendelee
kuchat nae mpaka badae kidogo au mbadilishie maada ili kukwepa huo mzinga ambao
unakuja mbele yako
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni