Jumatano, 19 Oktoba 2016

NDOA ZA SIKU HIZI UTASIKIA...WAMEACHANA!

Vijana wengi wanatamani kuoa na wasichana wengi wanatamani kuolewa. Mimi ni miongoni mwa vijana wanaojiandaa kuoa na hivyo niko katika kipindi cha kuyatafakari maisha ya ndoa.

Jambo moja ambalo limenishangaza ni wimbi la kuachana wanandoa. Asilimia kubwa ya marafiki na jamaa zangu walionitangulia kwenye ndoa hawako pamoja leo hii. Siyo wadada wala wakaka ukija kusikia eti walishaachana. Tena wapo waliokuwa wanapendana sana kiasi kwamba niliamini ni kifo tu kingewatenganisha lakini leo hii nasikitika kusikia wameachana.

Tatizo ni nini wakuu? Zamani watu walikuwa wanaachana lakini siyo sana kama siku hizi make ilikuwa ni aibu kuachika na baadhi ya makabila mtoto wa kike alikuwa anaambiwa akiachika asirudi tena kwao, kwa lengo la kumfanya aiheshimu ndoa yake na awe mvumilivu.

Baadhi ya watu wazima wameniambia kuna tatizo la feminism, wanawake wengi hasa wenye vipato wanapenda kushindana na wanaume hawajishushi kama wanawake wazamani ambao hata wakipigwa walikuwa wanavumilia tu.

Pia michepuko ya wanaume ni tangu zamani lakini siku hizi mwanaume akichepuka na mwanamke naye anataka kuchepuka ili alipize mwishoe ni kuachana tu.

Kingine watu wamepungukiwa na uvumilivu, juzi nimepigana sana kuokoa ndoa ya mdogo wangu ambaye alitaka kumuacha mkewe waliyezaa naye watoto wawili ili aoe kabinti ka Chuo Kikuu bila sababu zinazoeleweka lakini mwishoe nikabaini huyu amemchoka shemeji tu. Wanawake nao mwanaume akichoka mathalani hana hela tena au kaishiwa nguvu za kiume wanaanza visa mwishoe wanakimbia.

Nini sababu nyingine zinachangia? Karibu mtoe maoni tuwaandae vijana kabla hawajaingia kwenye ndoa takatifu.


Joyce:
Binafsi i don't believe in marriage japo nipo kwenye ndoa ila anytime ntaiacha maana ninayokutana nayo ni makubwa na si swala la uvumilivu no mimi nimevumilia kwa miaka minne unaenda wa tano ila mtu ndo kama anakuona unajipendekeza na huna pa kwenda, nadhani kiburi cha pesa na hulka ya mtu binafsi kuwa na wanawake wengi pia vinachangia ndoa nyingi kuvunjika,mwanamke unaweza ukavumilia na kujaribu kumrekebisha ila mwanaume anakuona km unampanda kichwani na kumfatilia mambo yake so hapo ndo kuna tatizo

Aron :Binafisi nikweli ndoa za zamani zili dumu nikisema mazingira ya kipindi iko yali luhusu,unakuta mwanamke tangu aolewe anashikwa kiuno na mmewe pekee ila nambie saivi hali ilivo.kwa wanaume sasa ndio usiseme.Kipindi iki ndoa zina changamoto kupita kiasi.

Kiukweli tuache kufalijiana ndoa za kweli ndio zinaishia.

Wanao sema ndoa raha waulize wamepitia matatizo mangapi bado wakaiona ndoa ni raha.

Kwa ufupi naamini miaka ijayo mtu mwenye akili timamu(ukiacha hawa wanao funga ndoa kuepuka dhambi ya zinaa) atakae kua kwenye ndoa atashangaza sana.



1.    NDOA za siku hiz tunavumiliana tuu tukichokana Tuna Achana Ndoa zilukuwa zile za Ma Babu zetu na Bibi zetu sio hiz za kuoa au kuolewa kama fashion tuu
Ndoa ni tendo la kiimani hivyo wanandoa inawapasa kumtanguliza Mungu mbele ili aweze kuilinda ndoa yao. Vijana wa siku hizi wakimaliza kuoana hawamuhusishi tena Mungu wao,, Hawaendi Misikitini wala Makanisani. Hawasali pamaoja! Sala ndio nguzo pekee ya ndoa! Muwekeni Mungu wenu mbele nanyi mtaishi miaka mingi kwa raha daima!


Pia vijana waache kuhusisha maisha ya ndoa na mambo ya social networks.. Social networks ndio chanzo kikubwa cha kuvuruga ndoa nyingi! Wana ndoa wanapotaka kuiga mambo ya watu wengine wanayoyaona kwenye social network ndio tatizo linapoanzia hapo. Mdada anaona mwenzake kila siku katolewa outing na mumewe naye anataka mumewe amfanyie vivyo hivyo bila kujali mpangilio wao wa kimaisha yeye na mwenza wake!

Jumanne, 18 Oktoba 2016

UNAIJUA DAWA YA MIGOGORO YA NDOA?KWA WANAUME TU!

Kwa wanaume ambao wapo kwenye ndoa na kila siku ugomvi ndani ya nyumba hauishi nimegundua dawa ambayo itarudisha amani na upendo ndani ya nyumba.

Ofcoz huitaji kwenda kwa waganga wala wapiga ramli cha msingi ni kuongeza mke wa pili, nakuhakikishia mke wa kwanza ataonyesha upendo ambao hujawai ona huku akikupa kauli nzuri nzuri ambazo hazikeri, lakini hujue hayo ni mashindano kila mmoja atafanya hivyo ili kuhakikisha unampenda yeye tu hivyo mitafaruku katika nyumba kutokuwepo.


Kama utabisha nenda Usukumani, Newala, Kigoma, Umasaini, Zanzibar, Tanga nk, utagundua kuwa kote huko wenye wake wawili wanaishi maisha ya amani zaidi kuliko mwenye mke mmoja.

TAFITI YA WAKE ZA WATU WANAOCHEPUKA!

Habari ya asubuhi wapendwa,
Kwanza kabisa naomba kutoa angalizo kuwa utafiti huu nilioufanya kwa takribani miezi miwili ilopita ni utafiti huru na usichukuliwe kwa mlengo wowote huo; dhamira ya tafiti hii ni kuifanya jamii iamke juu ya kuimalisha kwa mahusiano yaliyomo ndani ya familia zetu.
Kama kichwa cha habari kisemavyo; dhamira ya tafiti hii ilikuwa na lengo la kuibua na kuona kwa nini kwa takribani miaka ya hivi karibuni kumetokea ongezeko kubwa la watu waliopo kwenye ndoa kulalamika na hata kufikia kutoka nje ya ndoa na kuanzisha mahusiano mengine mbali na yale anayoendeleana nayo.
Mtafiti katika tafiti hii ametumia respondents halisi ili kupata picha kabili, na ifahamike kuwa utafiti huu umefanyika katika mikoa 5; Dar, Arusha, Mwanza, Iringa na Mbeya. Jumla ya respondents 50 kwa maana ya kuwa 10 kutoka kila mkoa walihusishwa kwa utafiti huu.
Kama nilivyotangulia kusema; utafiti huu ni halisi na sio wa kutunga au kubashiri, mtafiti aliweza kutumia main respondent mmoja (mwanaume) ambae ndio alitumika kuhusika moja kwa moja kwenye kufanya utafiti huu.
Utafiti huu ulihusika kwa main respondent (mwanaume) kujaribu kuwatongoza wanawake 10 kutoka kila mkoa, na endapo kama amefanikiwa basi alitakiwa kumalizia zoezi la kulala na wanawake hao kwa nyakati tofauti.
Uchanguzi wa sample size ulifanyika "kiholela" bila kujali aina ya mwanamke atakaekutana nae ambaye ni lazima awe mke wa mtu.
Tafiti inaonesha kuwa kila wanandoa wanawake 10, sita kati yao walikuwa wanakubali kutoka na kulala na respondent hiyo, tafiti ilienda mbali zaidi na kuangalia kwa nini wanawake waliopo kwenye ndoa wamekuwa ni rahisi zaidi kutoka nje ya ndoa ni kuwa; wengi wao asilimia 52 wamedai kuwa wanaume wao hawawaridhishi katika kuwapa haki yao ya ndoa; asilimia 12 wamesema kuwa wamegundua wanaume wao kuwacheat na wao kupelekea kurevenge, asilimia 16 wamesema kuwa waume zao wapo busy kiasi kwamba wanakosa haki ya ndoa, asilimia 14 wamesema kuwa waume zao wapo mbali na familia kwa kipindi kirefu hari inayopelekea wao kutoka nje ya ndoa na asilimia 6 wamesema wao ni tabia yao wanajisikia kuwa na mwanaume wengine mbali na mme wa ndoa.
Mtafiti aliona ni vyema kutoa angalizo kwa wanandoa, wote waume na wanawake kutokana na sababu mbalimbali zilizoelezwa na wahojiwa (respondents).

Nawatakia wakati mwema nyote

AINA 10 ZA HUSBAND WANAO KERA NYUMBA ZAO!

Kila ndoa inachangamoto zake na maana halisi ya ndoa ni ule uwezo wa wanandoa kuvumiliana katika changamoto hizo. Kuna changamoto za kimungu ambazo wanandoa hawawezi kuziepuka lakini kuna zile za kiuanadamua mbazo nyingi ni za kimakusudi na mtu huamua tu kuwa hivyo. Katika kuangalia ndoa leo nimeona nichambue aina kumi za waume ambao wake zao wanakereka kuwa nao;

(1) Wanaojiona kama Wafalme (King Husband);

Hii ni aina ya wanaume ambao hutaka kusujudiwa kama wafalme na hupenda kuwafanya wake zao kuwa kama watumwa. Hawafanyi chochote ndani ya nyumba kazi yao ni kutumatuma hata kama mke anaumwa atapaswa kuamka na kupika, wanataka waheshimiwe wao tu na mwanamke akikosea kidogo ni maneno au kipigo. Mwanamke hana kauli ndani na mume akiingia nyumbani ni kama bosi anavyoingia ofisini, wote kimya hakuna hata kuongea.

(2) Wanaume wanaojihisi bado hawajaoa (Bachelor Husband);

Hii ni aina ya wanaume ambao hawawashirikishi wake zao kwa chochote. Hufanya mambo kama vile bado hawajaoa, hutumia muda wao mwingi na marafiki zao wakifanya mambo ambayo mke hata hayajui, mke anaweza kustukizia tu mume kanunua gari bila kumshirikisha na mume haonyeshi hata kujali kuweza kumshirikisha. Hajali kama ana mke na mda mwingi huutumia akiwa na marafiki kufanya mambo yasiyo na msingi ambayo hayana mnanufaa yoyote katika ndoa yake.

(3) Wanaume wenye gubu (Acidic Husband);

Hawa hukasirika kila mara tena bila kua na sababu ya msingi, mambo hayaishi, kosa la mwaka juzi anaweza kukukasirikia leo. Wamemuudhi kazini hataki kusemeshwa na mnanuniwa nyinyi, mwanamke akiomba hela ya chakula ni shida ni kununa kutwa nzima, wanahasira na nirahisi kumpiga mke.

(4) Mume wa kila mtu (General Husband);

Hawa wanajifanya wasamaria wema, wanajali kila mwanamke, wanajali marafiki wakike wa mke na wakwao kuliko wanavyowajali wake zao. Mke anaweza kuwa na shida akasema hana hela lakini rafiki akampa. Wana marafiki wengi wakike na mara nyingi huwa hawaachani kabisa na ma X wao, wakiwalalamikia wanawasaidia kuliko hata wanavyowasidia wake zao wakati wakiwa na shida.

(5) Wanaume wanaojifanya wagumu (Dry Husband);

Hawa wanajifanya wagumu sana, hawana yale mambo ya kimahaba na wao hujua kuwa ndoa ni kuleta chakula tu na kushughulika kitandani. Hakuna kuongea na hawajali hata hisia za mke, mke akiongea kwao wala hawajali wanajifanya ni vidume sana na wanaona mambo kama vizawadi, kupiga simu, kutuma sms, kusema nakupenda, kununua maua ni mambo ya kike, yaani hawaonyeshi juhudi yoyote kuwafurahisha wekea zao.

(6) Wanaume wanaopenda kutumia wake zao (Panadol Husband);

Hawa huwa wanaume pale tu wanapokuwa na shida, wanakuwa na wake wazuri wanaowajali lakini wao wala hawajali. Wanapomhitaji mwanamke, wanapotaka mwanamke awafanyie kitu flani basi huja na maneno mazuri na hata kuleta vizawadi, wanajua udhauifu wa wake zao na huutumia kuwalaghai kuwatimizia mahitaji yao lakini wanapotimiziwa tu basi husahau hata kama wanawake, hawajali tena.

(7) Wanaume ambao hawataki kukua (Baby Husband);

Bado wanatabia za kitoto, hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe mpaka kuuliza kwa ndugu zao, mtu kaoa lakini kila siku humpigia simu Mama yake kuuliza hiki na kile. Yaani wakiongea kitu na mke nilazima aulize ndugu kwanza ndiyo kipitishwe na mke akifanya kosaakidogo kazi nikulinganisha mke na ndugu zake, mbona flani alifanya hivi, flani anaweza fanya zaidi na mambo kama hayo. Kwa kifupi hawawezi kufanya maamuzi na mkewe, ndugu zake hasa Mama yake anakuwa kama shemeu ya ndoa.

(8) Mume Mtalii (Visiting Husband);

Hawa wanakuja nyumbani kama wageni vile, mume ataihudumia familia yake kwa kila kitu lakini hawezi kuipa muda wake. Akirudi mke na watoto wamelala ni kugonga na hana sababu za msingi za kuchelewa, hata mwisho wawiki hupenda kutumia na marafiki au ndugu lakini si na mke. Hakuna kitu cha pamoja ambacho anafanya na mkewe au watoto wake, kila akiingia tu anakua na safari ya kutoka yaani hata atoke akakae nnje tu lakini si kukaa na mke au watoto.

(9) Wanaume wanaofuatilia kila kitu (Stalking Husband);

Hii ni aina ya wanaume ambao hufuatilia kila kitu, huchunguza kila kitu mwanamke anachofanya na hawampi pumzi. Akienda sehemu atachunguza anaenda na nani na alikutana na nani, huwa na wivu wa ajabu ajabu na kila saa huhisi wake zao ni wasaliti. Kila mtu mwanamke anayeongea naye wa jinsia tofauti huhisi ni mchepuko na hata marafiki wa mke wakike pia huhisi wanamkuwadia, kwakifupi hampi pumzi mwanamke.

(10) Mwanaume mbahili (Miserly Husband);

Huyu anaweza kuwa na hela lakini mbahili ajabu. Akimpa mwanamke hela atafuatilia matumizi yake mpaka senti ya mwisho, anafuatilia mpaka mambo ya jikoni. Sukari ikiisha anataka ajue iliisha ishaje na kila mara huhisi mke anamuibia hela labda akajenge kwao, huwa msumbufu sana na mgumu kutoa hela. Mwanamke akifikiria mchakato wa kuomba hela kwa mume hukata tamaa na wakati mwingine kuamua tu kukaa kimya na matatizo yake.


Hiyo ni baadhi tu ya aina ya wanaume ambao wanawake wengi wasingependa kuwa nao. Kama mwanaume upo hivyo jua mke wako hafurahii na anavumilia tu. Ndoa ni furaha amua kubadilika na usimfanye mke wako kuishi na wewe kwa kujilazimisha. Kama ni mume jiulize uko namba ngapi hapo na kama ni mke mezea namba ya mumeo.

WADADA ACHENI HIZO!

Hii tabia ya watoto wa kike kuvaa kanga moko na juu blauzi bila bra ndani  yaani ni balaaa mnatuumiza jamani!
Yani unakuta bidada  kajiachia njiani na kanga moko ndani hana chu**pi tu kalio tentemete!linatikisika kufuata miondoko ya bidada! siku hizi mnatembea kwa madaha na kujishebedua na unajua kabisa niko nyuma yako mkanda nje naelekea ofisini, ndo kwa makusudi unaregeza kanga halafu unaifungua hili uikaze eti, huku mjomba nimeshasoma ramani  yote kuanzia milima mpaka mabonde,masihara hayo!
Mna mpango madhubuti wa  kutupima mihemko yetu sisi wanaume marijari na wenye familia zetu tena hasa pale mnapojifanya mnaenda dukani , sokoni au saluni.
Mnatutesa jamani!unakuta mtu nimeokoka vizuri tu mnaanza majaribu! majaribu!
Hii tabia imeongezeka sana bila kujali maslahi ya watu na ndoa zao!
Mtuache sisi wengine ni waume za watu na tunaheshimu sana ndoa zetu hata kama zina migogoro!
Mtuache tuishi kwa amani hii migogoro ya ndoa ipo tumeizoea!
Mihamala imekata!

Mkome!