Jumatano, 10 Februari 2016

SHEMEJI KAKOMAA HALIPI DENI!

Nina jamaa yangu wa karibu sana tangu tukiwa hatujaoa kimaisha bado yeye mambo kumnyokea kama mimi imekua namsaidia sana kwa kumkopesha hela azunguishie kwenye biashara yake alafu mwisho wa mwezi unirejeshea n aka riba kidogo.
Sasa mkewe ni mfanyabiashara, na nna ukaribu nao wote wawili, watu wa mkopo sijui ni sijui BEY POTII  walikuja saloon kwake kukamata vitendea kazi kwa kua hakupeleka marejesho, ndipo akanipigia simu nimsaidie, 400,000/= ili wasichukue vitu, kuwa atanirudishia, nikamtumia hapo hapo kwa M_pesa
Basi siku moja akaniita nyumbani, nikaenda nikijua mshikaji nae yupo, na pia nikajua naenda kupewa hela, nasikitika kufika pale bila ya kusita alinikaribisha kinywaji (anajua natumia kunyagi kubwa na nyama choma bar ya jirani )huku akinambia nimsubiri rafiki yangu anakuja atanipa hela.
Kwakuwa tulikua tuna lamba kinywaji kunyagi kubwa ilipobaki robo mara shemeji aliinuka kuelekea jikoni mtandou  dhambi, ila nn yy ndie alinirubuni na kunishawishi, mm sikua na nia hiyo, nilimkuta kajifunga mtandio aliouvaa ukadondoka na kajazia ila balaaa!yaani ni lawama tu!Nikaona kyupi tu!Akaangua kicheko!
Akarudi uku akiomba msamaa kiuongo uongo  tukaendelea na kunywa kinywaji  mara ya pili akainua tena na kwenda nje mtandio ukaangua tena chini akiwa mtupu bila hata ya kufuri!Nikajikuta nimeanguka kwenye dhambi nae!Tukamalidha nikaamua kuondoka jamaa asinifume!
Tumeshatenda dhambi kama mara tano hivi, na sasa hivi kasema nikiwa namuhitaji niwe namueleza tu tunaenda sehemu tunamalizana ila hela yeye hela  hana, kwamba hadi nitakapochoka mwenyewe au nitakapoona hela imeisha.
Sasa wadau kwa hali hii nitapataje hela yangu na mimi nimeitoa kwenye mzunguko wa biashara, mshikaji analijua hili deni maana siku watu wa mikopo walipoenda kukamata vitu vya mkewe yy ndie alimshauri anijaribu mm, sasa hivi nikimkumbusha mshikaji deni anasema nimwambie mwenye deni mwenyewe.

Sasa hizi ndugu zangu si lawama? Au niendelee tu kupumzika na mkewe hadi nitosheke?

UKIENDA NA MKE WAKO UKWENI(KWAO) USILALE NAE MBALI

Mahali ninaposhi kuna nyumba zipo kama tatu hivi ndani ya ua mmoja ,sasa jana jioni nilivyorudi kutoka kazini niliitwa na mke wa jirani kujaribu kusuruhisha ugomvi  kati ya mume na mke ingawa baada ya wao kutoka rikizo ,hatukufanikiwa kwani mwanaume aligeuka mbogo na pasipohitaji suluhu yoyote na mkewe,
Kisa kilikua hivi ,wakati wakiwa wanatoka likizo kwa wazazi wa mwanaume waliamua kupitia kwa wazazi wa mwanamke japo kukaa hata siku mbili yaani ukweni kusalimia, sasa zogozogo lilianza hapa, baada ya kufika kwao mwanamke, walikaribishwa vizuri na wakaoga, wakala na sasa ikafika zamu ya kwenda kupumzika. Sasa mwanamke kumbe alikuwa ameshamtaarifu boyfriend wake wa siku nyingi hapo mtaani kwao kwamba nitakuja siku fulani, siku hiyo wakati wa kulala, mwanamke alikataa kulala na mumewe ndani ya nyumba yao ( (nyumba ya ba mkwe), eti akidai (mwanamke) kwamba siyo vizuri kulala pamoja eti yeye na mumewe kitanda kimoja kwenye nyumba ya baba yake, akihoji je, ikitokea "mwanaume akahitaji mchezo itakuaje?Kwani mwanamke huwa anapiga sana kelele wakati wa tendo na wazazi watasikia”!
Basi jamaa (mumewe) ikabidi awe mpolekwa shingo upande  akamruhusu mkewe akalale chumba kingine lakini ndani ya nyumba hiyo, sasa mkewe akatumia mwanya huo, kufungua mlango na kwenda kwa ex boyfriend wake wa muda mrefu, anaekaa nyumba ya tano kutoka kwao kwa bahati mbaya mambo yalinoga sana usiku akajisahau mpaka saaa kumi na moja alfajiri akarudi .
Wakati anarudi akakutana na baba yake nje ( ambaye ni ustaadhi  akijiandaa kwenda  swala) nje, ndo baba yake akaanza kumuuliza anatoka wapi usiku huo na yupo peke yake, mumewe yupo wapi! Kumbe wakati anamuhoji mkewe, mume  alikuwa macho akupata usingizi alisikia kila kitu maana dirisha la chumba alicholala mumewe lipo upande wa getini, mke wake alishindwa kutoa jibu lolote  huku akiomba radhi kwa baba yake tena kwa sauti ya kunong'oneza sana.

Kulipopambazuka mume aliamua kupiga kimya akapotezea na alikaribishwa chai akanywa na baadae akaomba kuondoka ili kuwahi kazi akidai likizo yake ilikuwa imekwisha.Wakaondoka pamoja na mkewe, sasa kufika nyumbani ndo maswali yakaanza.
Ndio zogo kubwa likafumuka kwa jirani , na ikabidi mwanaume ampe nauli mkewe arudi kwao kwanza ili atafakari hatua nzuri za kuchukua dhidi yake.

Kiufupi, Mwanamke alikomaa bila ya kukubali kosa, alikataa ila mmewe alipomuuliza swali aliloulizwa na baba yake juzi na jibu ambalo yeye alimjibu baba yake ndipo mwanamke akaishiwa nguvu,na kuanza kuangua kilio kikbwa tukadhani kuna msiba!Mumewe alimwambia nguo aliyovaa siku hiyo ya alfajiri na baba yake alivyokuwa amevaa siku hiyo ya alfajiri.

Sasa ndugu zangu wanaume kazi kwetu kwa wale mliooa tayari kazi kwenu, sisi wengine tunajifunza kwanza. Jana baada ya kutoka kazini, nilikuta ugomvi kwa jirani yangu ambaye alikuwa ameenda likizo na mkewe sasa wakati wanataka kurudi kazini ikabidi wapiti kwao mwanamke kuwasalimia, sasa zogozogo lilianza hapa, baada ya kufika kwao mwanamke, walikaribishwa vizuri na wakaoga, wakala na sasa ikafika zamu ya kwenda kupumzika.

Sasa mwanamke kumbe alikuwa ameshamtaarifu boyfriend wake wa siku nyingi hapo mtaani kwao kwamba nitakuja siku fulani, siku hiyo wakati wa kulala, mwanamke alikataa kulala na mumewe ndani ya nyumba yao binti (nyumba ya ba mkwe), eti akidai (mwanamke) kwamba siyo vizuri kulala pamoja eti yeye na mumewe kitanda kimoja kwenye nyumba ya baba yake, akihoji je, ikitokea "mwanaume akahitaji mchezo"?

Basi jamaa (mumewe) ikabidi awe mpole amruhusu mkewe akalale chumba kingine lakini ndani ya nyumba hiyo, sasa mkewe akatumia mwanya huo, kufungua mlango na kwenda kwa ex boyfriend wake wa muda mrefu, akarudi asubuhi ya saa 11 alfajiri.

Wakati anarudi akakutana na baba yake nje, ndo baba yake akaanza kumuuliza anatoka wapi usiku huo yeye peke yake huku akihoji mume wake alipo! Kumbe wakati anamuhoji mkewe, mumewe alikuwa anasikia maana dirisha la chumba alicholala mumewe lipo upande wa getini, mke wake alishindwa kutoa majibu yoyote huku akiomba radhi kwa baba yake tena kwa sauti ya kunong'oneza sana.

Kumbe mumewe alisikia yote na alipoamka alikaribishwa chai akanywa na baadae akaomba kuondoka ili kuwahi kazi akidai likizo yake ilikuwa imekwisha.Wakaondoka pamoja na mkewe, sasa kufika nyumbani ndo maswali yakaanza na ugomvi mkubwa umetokea jana, na ikabidi mwanaume ampe nauli mkewe arudi kwao kwanza ili atafakari hatua nzuri za kuchukua dhidi yake.

Kiufupi, Mwanamke hakukubali kosa, alikataa ila mmewe alipomuuliza swali aliloulizwa na baba yake juzi na jibu ambalo yeye alimjibu baba yake ndipo mwanamke akaishiwa nguvu, mumewe akamwambia nguo aliyovaa siku hiyo ya alfajiri na baba yake alivyokuwa amevaa siku hiyo ya alfajiri.


Sasa ndugu zangu wanaume kazi kwetu kwa wale mliooa tayari kazi kwenu, sisi wengine tunajifunza kwanza.

NIMETUMA MESEJI HII KIMAKOSA KWA MAMA MKWE!

Habari zenu wapendwa,

Natumaini  mpo salama japo kwa upande wangu sipo salama sana nimechanganyikwa leo mbayaaaa!mpaka ninavyoandika uzi huu nimeshindwa hata kwenda kazini na hapa moyo wangu unaenda mbionaombeni msaada kwenu  wa kiushauri na wa kimawazo naweza hata mkanipoteza katika dunia hii kwa presha niliyokua nayo hapa nilipo ,nimeshindwa hata kuwasha gari !akili zangu nahisi hazipo timamu kwa sasa!
Ukweli ni kwamba nilikuwa naandika SMS kwa mchepuko wangu uitwao Roswita au (mama Jane) na kwa bahati mbaya sana wakati natuma nikakosea namba na kutuma katika namba ya mama mkwe wangu na meseji ikawa sent and delivered.Kwenye simu yangu nimesevu jina lala Mama Jane sasa kwa kuwa jina lipo karibu na jina la “mama mkwe” nikajisahau na kubonyeza sent alafu OK kwa bahati mbaya!Nikajikuta tayari meseji ipo kwenye sent item na mara baada tu ya kituma ghafla mama mkwe akanipigia zidi ya missed call ishirini hivi  ila kwa kuogopa na aibu nimeona nisipokee na nimezima simu kabisa.

Na kwa dalili ninazoziona ni lazima tu atakuwa ameshamtaarifu na pengine hata kum-foward ile SMS mke wangu Magie maana nampigia simu hapokei ila amenitumia meseji inasema “sasa ndo umefanya nini mume wangu!” sasa sijui leo kama patakucha akiludi baadae  maana ndo ameshakwenda kuwajibika tayari kazini.

Meseji yenyewe niliyoituma ni hii " Mambo vipi Roswita Bonita ! Hujambo? Umeamka salama? Vipi si tayari umeshamaliza period yako na leo naweza kuja ukanipa mambo love?unipe na ile tamu tamu honie!Zingine nizibakize kwa dada yako “baby wife” wangu maalum kwa siku ya Valentina  Jumapili hii kwani ni haki yake ya kindoa. Utaninunulia Wine gani leo ili nikuchangamshe vizuri kama unavyopenda?Honie usisahau na yale mafuta basi!Baby uvae ile bikini ya purple na mechisha na ile bra yake! Halafu ulisema unataka hela sijui ya kununua nguo ila kwakuwa ili li mke langu nalo eti linataka hela sasa ngoja kwanza nilidanganye kuwa sina na lisubiri hadi nipate ila wewe mke mdogo  nakutumia sasa hivi sawa? Si ulitaka Tsh laki 1? Sasa nakutumia Tsh Laki 2 na nusu hizo zingine utajua utanunua nini au utaitumiaje sawa baby?
 Nijibu na tambua sitokuacha kamwe mwaaaaaah Loswita ".


Hiyo ndo meseji niliyotuma najua kimeshanuka sijui nikimbilie wapi?Nilipiga simu kwa jamaa yangu yupo Telecom company ikiwezekana aisimamishe iyo meseji hewani nimpe hata laki tano imeshindikana kabisa!mnijibu haraka basi ili niweze jipanga kuzipangua hoja kama hali ikiwa mbaya kweli.

Alhamisi, 4 Februari 2016

SIJAMUELEWA WIFE JUZI!

Nimefika kazini mapema leo kama kawaida yangu,najitahidi kufanya kazi yaani hata mambo hayaendi nashika hiki mara naacha naenda uani haja haipo narudi naangalia computer yaani  hakuna kinachosegea!mawazo tele moyoyni!Sasa nikiwa katika kutafakari kuna jambo nimelikumbuka limenichanganya kidogo....
Huwa tuna kawaida ya kila weekends mimi na mke wangu kufanyiana usafi ikiwemo kunyoana nywele za chini na makwapani. Huwa tunafanya hivi weekends...
Sasa imepita kama mwezi hivi nilikuwa busy sana sikumnyoa. Sasa jana usiku nimetoka kazini akaning'ang'ania nimnyoe na hakutaka kabisa kusubiri weekend. Mzee mzima nikachukua kinyoleo nikaanza kazi huku namtania tania na kumtekenyaa hapa na pale..
Sasa kinachonichanganya ni hiki. Wakati namyoa nikabakisha vinywele flani nikamtania kuwa hivi tuviache nitamalizia weekend. Akanijibu..
                                                                     
"Mmmh malizia baby  si nitaonekana kituko mie"

Nikashtuka kidogo alafu nikapotezea  kwa kubadilisha stori nyingine, nikammalizia, tukaoga tukalaa. .Sasa wakati natafakari mambo yangu hapa job ndo nikaimbuka ile statement yake.

"Mmmh malizia baby si nitaonekana kituko mie"

Hivi sijui alimaanisha nini...ataonekana kituko na nani?

Mbaya zaidi nampigia hapatikani na nimeondoka simu yake ina chaji full maana alitumia chaja yangu usiku mzima...

Sijui niombe ruhusa naumwa nirudi nyumbani?

Au shetani tu ananiletea mawazo mabaya?

Hivi inawezekana kweli mke wangu akawa anagegedwa nini?Keruuuu

Jumatatu, 1 Februari 2016

WIFE KAKUTANA NA EX WAKE KAFURAHI HAKUNA MFANO!

Wadau mambo vipi?
Kuna jambo limeikoroga akili yangu sana juzi naomba niwashirikishe kidogo. Jumamosi iliyopita mimi na wife tulienda kula bata maeneo ya Villa Park hapa  Mwanza nyakati za jioni baada ya kutoka kufanya shopping hapo Rock City Mall maeneo ya Ghana. Wakati tumefika maEneo ya Nyegezi tukielekea mjini wife alinambia nisimame kidogo kuna rafiki yake yupo saloon ambaye nilikua namfahamu tangu wakiwa chuo Saut  Nyegezi , nae alikua anaelekea hukohuko Rock cCity Mall tumchukue, akampigia girlfriend simu aje barabarani . Hivyo tukawa watatu kwenyegari mpaka  mizunguko ya huko mall; mimi, wife na girlfriend ambae alikua family friend kwetu ingawa mimi sina mazoea nae kiiivile.
Kwa kuwa ilikua mida ya saa kumi na moja jua lilipoanza kuzama tukaamua kukaa Villa Park kwa ajili ya kusubiri kusakata rhumba na kwa kuwa wwife huyu alikua ni shaga yake hasa sikua na option zaidi ya kuwaacha wahe huru uku mimi nikiendelea kugonga Konyagi yangu kubwa na better lemon  na wao walikua wanakunywa Saint Anna moja wawili, tukakaa karibia na kaunta ya chini  nje. Kwenye saa mbili kasoro usiku akajitokeza jamaa mmoja kwa sura simjuhi kabisa ,baada ya kutuona akaja kutusalimia, ambapo wife aliinuka kwa shangwe kubwa na kumlaki kwa hugs na zile kiss za mashavuni wanazopiganaga wale wanaojifanya wazungu,jamaa likamkumbatia wife kwa nguvu.Nilipata kawivu kidogo lakini nikajikaza kiume!
Wife akanitambulisha kuwa "he is a longtime friend,huku nikiendelea kumtazama kwa mashaka kwani nilihisi zile mbwe mbwe zote za kukumbatiana pale kuwa sio ‘genuine’ lazima kuna kitu au kulikua na kitu fulani zamani,haiwezekani,hamna hapana!kuna kitu tu!". Jamaa akaita weita na akazungusha mbili za vinywaji, alafu akaniomba aende akamtambulishe wife kwenye meza yao kwa rafiki zake ,sikupendelea hiyo hali lakini kwa kuwa nilimuona wife ana muhemko fulani wa bashasha ya kukutana naa “friend wa zamani” nikakubalitu kwa shingo upande  ingawa moyoni nilikua nimefura kwa hasira, sema sikutaka kuonesha, bahati mbaya zaidi meza ya hiyo aliyokua ametokea huyo jamaa  ilijaa wanaume pekee.
Tukabaki wawili wakati wife anaongea na meza ile, yule girlfriend akasema "shemeji naomba namba yako hapa mjini huwezi kujua ya kesho na keshokutwa", nami nikajibu ni kweli kabisa, tukabadilishana namba.Monday yule binti akanipigia simu nikiwa kazini akaniambia shemeji kuna jambo nataka kukuambia ila usinitaje, nikajibu poa, akasema, "Yule jamaa wa jana ni ex wa mkeo. Walikua wapenzi kwa miaka yote mitatu chuoni wakiishi chumba kimoja nje ya chuo kama mke na Mume".
Na kwamba kwa kipindi chote cha hiyo 3 yrs alitoa kama mimba 2 hivi za huyo mshikaji, pia uhusiano wao ulienda hadi mtaani after university life. Walikuja kuachana kila mtu alipopata kazi yule ndugu akapelekwa Songea. Since then hawajawahi kuonana hadi hiyo jumapili pale Lock City Mall,Mwanza na kwamba ile njemba limerudishwa hapa Mwanza na halijaoa bado ila lina mapene sana.
Binti huyu alinibembeleza sana kuwa nisimtaje kabisa kama yeye ndie source ya hiyo habari. Huyu binti ni rafiki wa wife tangu chuo ila bahati mbaya ndoa yake ilipata shida kidogo na kushindikana kutokana na uzinzi wa mwanaume.Niliporudi home jioni ya monday nikaamua kulianzisha, ambapo wife alidai hakuona busara kunitambulisha kwamba yule bwana alikua ex wake.
Nikamuuliza ilikuaje ukafurahi na kushangilia kiasi kile na kushindwa kuficha kabisa hisia zako? Akabaki anajiuma uma tu na kushindwa kujibu.
Kiukweli sijaridhika na majibu yale na bado nafanya uchunguzi.



JINSI NILIVYOKWEPA CHANGA LA MACHO LA MIMBA YA MCHUMBA

Siku hizi limezuka wimbi kubwa la wanaume wengi kulea watoto ambao sio wao bila ya wao wenyewe kugundua yaani wanakuwa ni watoto wa goli la mkono , mara nyingi mwanamke humsingizia mtoto mwanaume yule mwenye malengo nae(kwa kiswahili cha mtaani tunaita  mwanaume wa display au wa shooting video ) au mwenye uwezo wa kulea mtoto yule, mara nyingi mimba za kwanza za ubinti huwa ni za kusingizia.
Nije kwenye yaliyonikuta mwenzenu miaka nane iliyopita nikiwa nimeajiriwa kwa mara ya kwanza kazi nzuri serikalini Agency mshahara mnono ata ata pombe sijaanza kuonja nilipata mpenzi mwanachuo akiwa chuo cha ualimu kabinti kazuri katamu yaani  nilikapenda sana huku nikijua ananipenda mara kwa mara alipokuwa anafunga alikuwa anakuja kwangu maana hata wazazi wake walijua uhusiano na mapenzi yaani ilikua mahaba niangamize!
Kuna kipindi alinilazimisha kuja kwamba huku akisisItiza kuwa amenimisi big time  nikamkatalia lakini akalazimisha kuja kumbe alikuwa tayari alikua na mambo yake ,akafika na kulala siku ya kwanza ya pili uku machale yakinicheza kwanini amelazimisha kuja kwa nguvu,kwaiyo mzigo sikula nikavunga kuwa naharisha tumbo .Mungu saidia siku ya tatu nae akaugua ghafla full kutapika halafu akawa analazimisha kuondoka nikamkomalia kumpeleke kwa nguvu hospitali nikamnong’oneza daktari aliyekua mshikaji wangu tulikua na mazoea ya kugonga “vyombo” bar moja jilani  kuwa  ampime vipimo lakini sanasana mkojo kucheki kwani nahisi ana “jipu” la mimba, majibu kutoka ana mimba kuumuliza akaanza kulia na kunieleza kuwa alichepuka na mwanachuo mwenzake mara akawa amebeba akaona anisingizie maana ananipendasana ,hahaaaaaaaa nilimtimua kama mbwa,ndio ikawa mwisho wa mimi na yeye.
Hivyo basi nawashauri wadogo zangu wa kiume kuwa ukiwa na mchumba ukaona analazimisha kuja kwako jiulize maswali mengi kwani wakati mwingine YES maana yake NO! ujue inawezekana kanasa huko anataka kukushikiza wewe kwasababu wewe ndo “husband material”cha muhimu akija mlie “taimingi” mpeleke hospitali au nunua kipimo na hakikisha mkojo anakojoa ukiwepo ili asikuwekee maji kwamba ni mkojo utapigwa mchanga wa macho Jombaa!

Kulea mtoto wa mwanaume mwingine inauma.

KWA WADOEZI WA WAKE ZA WATU PITIA HAPA!

Kuna dogo mmoja rafiki yangu (sio  kivile sana  ila tunaangalia mpira pamoja)  alikuwa anatembea na mke wa mtu kwa muda mrefu tu, Ila mke ni mkubwa kiasi sana kwa mshikaji, mke ana kama miaka 37 hivi alafu jamaa ana 30. Mume alikuwa bize sana na michakato ya kuboresha familia yake na kiukweli alikuwa anaihudumia familia yake vizuri tu hasaa mpaka akafanikiwa kumnunulia mkewe gari aina ya Harrier kwa ajili ya kutembelea nakuendea kwenye  kitchen party,huku mwanaume akiendelea kusota na madaladala kilasiku.
 Kutokana na huduma nzuri na kamili ambazo mke alikuwa anazipata hata muonekano wake kwa kweli ulikua unavutia hata huwezi kumdhania kama yupo above 30 na tayari ana watoto 3, kwani alikua amejazia vizuri tu wowowo limemwagika la haja tu ,nadhani matunzo mazuri na kutosimangwa na   mume kulimfanya azidi kunawili na kuwa  mzuri ukichukulia kuwa pesa ilikwepo na hana stress za daladala katikati ya  jiji la Dar es Salaam.Kipindi cha kampeni za uchaguzi mwezi uliopita alikua akivaa gauni la chama kimoja cha siasa zile alama zilikua zikimkaa vyema kwenye makalio yaani ilikua ni patashika barabarani kwa wapita njia na madereva wa bodaboba na teksi!Macho hayana pazia!
 Mahusiano yao sijui yalianzaje maana mimi niliyagundua kwa bahati mbaya tu baada ya kuona picha ya yule mama kwenye simu ya mshikaji akiwa amevaa bikini pekee, hapo nikapata mashaka na ndipo nilipomuuliza mshikaji hapo vipi tena ? akawa hana namna ikabidi aniambie ukweli wote, nikamshauri sana kukaa mbali na yule mwanamke kwani asije akahatarisha maisha yake na nikamwabia mbaya zaidi nayeye ana mke kwanini anafanya hivyo?Alinijibu kuwa namuonea wivu nikaona sio shida nikae zangu kimya na nikamwambia wazi kuwa urafiki wetu uishie hapo maana mimi sitaki matatizo na najua namna mke anavyouma,na nilimwambia hawezi maliza miezi sita bila ya kukamatwa   akauliza kwanini?nikamjibu kuwa ni lazima wataanza kujisahahu na kuhisi kuwa  wapo peponi na hakuna mtu atakayeweza kuona wanayoyafanya.
 Imepita miezi kama mitatu hivi tangu hayo yatokee juzi amefika ghetto macho mekundu  anataka nimsaidie hata ushauri.
Nikamuuliza ushauri gani tena?        
Akajibu kwamba  mwenye mke amegundua mchezo wa mkewe akatega mtego akawanasa, alipowashika akawaambia wavue nguo zote wafanye mapenzi huku akiwa anawarekodi video na kuwapiga picha nyingi nyingi pia na kumfanyia  mambo ya kinyama sana ila hajaniambia ni mambo gani,(sina uhakika kama “alimuwowa” au la) Mume amemwambia mshikaji amchukue yule mwanamke ampeleke aende kwao (kwa mwanamke) akaseme yote yaliyotokea na akaseme kuwa anataka aoe yeye then ampeleke kwao (kwa mshikaji) akamtambulishe kama mchumba wake(mke wa pili mtarajiwa) process za ndoa zianze na yeye atatoa 50% ya gharama zote ili akafaidi vizuri moja kwa moja, ametoa wiki 1 tu huo mchakato uwe umeanza otherwise atampeleka mahakaman maana ushahidi wote upo au atasambaza picha na video.

Amenifuata nimsaidie mimi sijui hata nianze wapi kumshauri, naogopa kumkashifu au kumkumbusha ushauri wangu nahisi nitamuumiza.. Wadau tunafanyaje hapo?Daah mke wa mtu nomaaa yaani sio kabisa  maze.

WADADA MUJIFUNZE KUWA NA SIRI BASI!

Najua wanawake siku hizi wana uhuru kuliko zamani lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa hata zamani wadada walikuwa wanajipa good timevilevile kama sasa ingawa teknolojia zinatofautiana.

Tatizo lenu wadada sikuhizi hamna siri!

We angalia kila kitu kuhadithia mashosti. Kila utakayetoka naye unaonyesha watu. Kila utakachopewa kila utakapopelekwa (i.e hotels,beach,outdoors) tutaona picha istagram,face book ,wengine ujisahau na kuanza kusifia mpaka gemu alilolopewa na fulani lol! bidada mmemzidi!
Sio tu utasababisha sasa kama ni bwanako akija kama ni kazini au hostel watu waanze kumwinda sasa!hahahaaaa pole utalia na wenzako watakula samba na wewe kimya kimya tena bila wivu!si umewaoneshea “windo” la Nyati aliyenona!
Kwani umezaliwa nao tumbo moja?. Ukipewa hela kila wakati wewe kutulushia mapicha sijui mara Splash Mlimani City ,mara Wool Worth Posta, mara Nairobi  five star kwani nasisi hatutamani kwenda uko?shauliyako bwanako huyohuyo nae tutaenda lalanae uko!
Wengine mnapelekwa guest tu lakini tutaona picha ya dinner na breakfast za kizaramo. Mbona wenzenu wanapelekwa 4 stars wamekausha!
JIFUNZENI USIRI.
Acha love,sex life yako iwe private. Ukiji praudi sana na kutooneshea mmeo akija tu lazima tujibinue makaliona kufungua vifungo viwili vya baluzi kifuani ooh! joto!habari ndo iyo!mumeo mume wetu sote!hahaahahaaa!
 Usihadithie mashosti,kwani kila shosti unaemuhadithia lazima atatamani nae kimya kimya !yaani moyoni ataumia wewe hutajua ila kosa moja magori mia!akikutana nae bwanako Mlimani City imekula kwako kwani ni full kujirahisisha tena siku hiyohiyo ataanza shemeji nina kiu ya bia nipeleke Calabash napenda sana live bendi!Wakifika uko shostito atajimwaga full kuachia mapaja wazi kwa shemeji ili bia ikikolea shemeji ajiongeze mwenyewe ikigoma hiyo utasikia nawewe unajifanya umepata mwanamke wakati  hana lolote si ni m#laya mwenzetu tu yule!Habari zake zote ninazoe niulize mie tena ukimshusha saloon huwa tunakuonea huruma!.
 Ukipitia,ukalala hotelini wakati unajua unaishi kwenu au hostel, au unajua unataka kuonekana mtu wa dini, achana na hiyo camera.
Usije shangaa kesho unaachika fasta baada ya mashosti kumjaza chifu maneno kuwa mwezi uliopita  mimba uliyotoa haikua yake bali ya mwalimu wa chuo alikunyofoa sup  au  dereva wa bodaboda wako!
Hupungukiwi kitu. Zoea kusema sina mtu sanasan nyie  wadada wa chuo mlio na pressure za kushow off mabwana. Itawasaidiasana.
**you wanna be "that" good lady at 30? Don't get caught at 20.
Afu wanawake tunajuaga kurushana roho jamani. Kuna mtu anaweza akakusimulia mambo yake kwa mfano, boyfriend wake anavyo mtreat kumbe muongo mkubwa.
Hii ilishawahi kutokea kwenye  bufee ya kampuni moja kubwa hapa Dar es Salaam wakati wa mlo binti alianza kuwarusha roho wenzake yupo kwenye foleni ya chaklula kuwa oooh baby niletee take away huku bufee la leo halihamasishi pitia Steers niletee beef berge mbili ……
Sasa kwakua mimi niliohisi anadanganya na namba yake ya simu nilikua ninayo nikamtwangia simu hapohapo kwneye foleni kwanini simu isilie sikioni kwake uku anaongea!watu wote walishikwa na butwaa na kuanza kucheka !

“Mmmmh Jack muda wote unaongea na dear kumbe uongo!”
 Ndo wale wanaojinunulia hadi zawadi afu anadanganya wenzie kanunuliwa na baby. Aonekane tu yeye ndo anapendwa sana, yeye ndo anaenjoy mapenzi sana mmh, akili kumkichwa. Unaanzaje kusimulia ulivyolala na mtu mmh? What for?
Uzuri wa haya maisha kila generation huona wazazi wao ni washamba na kwahiyo kamwe ma teenager wamiaka 20 ijayo hawatafanya upuuzi wowote tunaushuhudia hivi sasa God forbid
Nope kuna kukua kimwili, kiroho na kiakili ujue. So watakua tu kiakili siku moja


WANAWAKE MNAOPENDA KWENDA KWA WAGANGA WA KIENYEJI SOMENI HAPA!

Kuna jamaa mmoja namfahamu anapenda sana ngono na pia ana uwezo mzuri kipesa, sasa kuna wadada wengi alikuwa akiwatamani sana ila kuwapata ikawa ni ngumu kwasababu domo zege  alafu mvuto hafifu,alichofanya ni kwenda hadi kwa mganga mmoja maarufu sana ambaye wanawake wengi hupenda kwenda kwake, akampatia yule mganga mshiko wa maana  na kumwomba kuwa kila mwanamke mrembo anayefika kwake aidha kutafuta dawa ya kupata mchumba awe anaambiwa na mganga kuwa, ukitoka hapa mwanaume utakayekutana nae njia panda wa kwanza kukusemesha ,usimkatae maana huyo ndo anapata na mzimu wako wa mafanikio na uhakikishe umetembea naye tena ikibidi siku hiyo hiyo utafungua njia ya bahati katika mapenzi.
Baada ya kupanga mikakati yote na yule mganga, jamaa akawa anabana sehemu ya njia panda na  kusubiri mwanamke anayetoka kwa mganga na tayari wanakuwa wamefanya mawasiliano na mganga juu ya ujio wa uyo mrembo!, jamaa tayari kamaliza mabinti kibao!
Anakuwa amevalia mavazi tofauti tofauti  ili asitambulike na ana laini kibao za simu, anahakikisha kuwa kawalala siku hiyo hiyo.


Wadada mgeukieni Mungu kwa shetani hakuna kitu zaidi ya mauti.

TOFAUTI YA MWANAMKE MWEREVU NA MJINGA HII HAPA

Mwanamke mjinga:-

1. Anamkomoa mumewe.

2. Analala mapema kabla ya mumewe.

3. Anachelewa kuamka kabla ya mumewe.

4. Mbishi, anahisi kuonewa mda wote.

5.Anadhani kumnyima mumewe unyumba ni kumkomoa

6. Mmekaa sebuleni anahadithia tu mafanikio ya familia za watu wakati yeye ndo kigezo cha kero.

7. Hataki kuzungumzia mshahara wake.

8. We unajenga familia ye anajenga kwao

9. Mkikaa anaanza umbea ama kuponda ndugu na majirani.

10. Haridhiki (mwanaume unatoa jasho, ila ye anakudiscourage wakati Ye akishuka kwenye kochi anakaa Kwenye jamvi na baadaye anelekea saloon kupiga umbea. kuhusu lara 1 kafumaniwa gesti.

11. Nyumbani housegirl hapumziki. 1

12. Anajali ajira yake tuu na hataki kufuatiliwa mambo yake.

NOTE: Akikutana na mwanaume kichwa ngumu anamrudisha kwao ameshazalishwa watoto 3, anaenda kwa mwingine anaongezewa watoto 2, anazinguliwa anapigwa toto lingine na wajanja wa mtaani, unakuta kazaa na kila familia mtaani baadaye anaishi ghetto au kwao.

Mwanamke mwerevu;

1. Unaamka yeye kashaamka na kusema "baby amka maji ya kuoga yapo bafuni" (mwanamke adimu sana)

2. Unajiandaa kwenda kazini, nguo zishapigwa pasi (jamani hiyo kazi kafanya saa ngapi? unajikuta unaenda kazini upo kwenye daladala kimoyo moyo unamwambia "I love u honey"

3. Unarudi jioni unakuta anakuvua soksi, hujui hata atazifua saa ngapi maana huwa hujui anazifua saa ngapi?

4. Umejipumzisha kwenye kochi au kitandani mara kakukalia mgongoni anakufanyia masaji mgongoni, ( alijuaje unataka ufanyiwe masej? Unaishia kusema Thanks baby).

5. Kila anachotaka kufanya kujiendeleza anakuambia na unaweza kumpa mtaji mana ni mkweli (ni baraka kwenye familia)

6. Anapenda ndugu zako (siyo mama mkwe akija anasimamisha pua juu kama nyati anatafuta maji)

7. Anakupa moyo kwenye wakati mgumu, mf: umefukuzwa kazi anakushauri (baby hayo ni maisha tu, usijali utafanikiwa kama vipi tusimamie ule mradi wangu mpk uajiriwe).


NOTE: Hawa ndio type ya kuoa na kunyenyekea maana wanajielewa.

HIZI NDIZO AIBU NA MADUDU YA WANAUME WA KARNE HII!PITIA TAFADHARI

1. Japo maisha ni kusaidiana ni aibu na fedheha mwanaume kulishwa na mkewe.
2. Ni aibu na fedheha mwanaume kuhamia kwenye nyumba ya mkeo ukakala ukakoroma na taulo ukafunga.
3. Ni aibu na fedheha kuendesha gari la mkeo wakati wewe hujawahi kumiliki gari alafu unawaka wivu juu yake.
4. Ni aibu na fedheha kuishi na mwanamke ambaye wakwe zako wanajua kuwa anakuzidi uwezo.
5. Ni aibu na fedheha kumuoa mwanamke ambaye anamiliki uchumi wa familia hata watoto anasomesha yeye wewe unajivunia uume mkubwa na kwnenda chumvini sana.
6. Ni aibu na fedheha kila likizo unaenda kijijini kwa mkeo na watoto wote kisa yeye anazohela.
7. Ni aibu na fedheha kukaa miaka mingi unamlaumu mkeo kuwa hazai wakati wewe huna hata mtoto wa kusingiziwa.
8. Ni aibu na fedheha kumrudia mwanamke aliye kuacha yeye mwenyewe kipindi kirefu na akaamua kukurudia yeye mwenyewe tena kwa masharti kutoka kwake.
9. Ni aibu na fedheha kupewa zawadi ya kiwanja na wakwe zako siku ya send off.
10. Ni aibu na fedheha kujenga kwenye kiwanja cha mkeo wakati wewe hujawahi kumiliki kiwanja.
11. Ni aibu na fedheha kulelewa mtoto wako na baba wa kambo wakati wewe upo unaishi na unajiita kidume.
12. Ni aibu na fedheha kukaa kwenye nyumba yenye fenicha zoote kanunua mkeo.
13. Ni aibu na fedheha kusimamia ujenzi wa nyumba ya mkeo wakati wewe huchangii hata shilingi mia.
14. Ni aibu na fedheha kulea mtoto ambaye sio wa kwako kwa kisingizio cha kitanda hakizai haramu wakati mkeo anajua mtoto yule sio wa kwako.
15. Ni aibu na fedheha kulala kimapenzi na mwanamke ambaye anajua kuwa wewe unajua na unaushahidi wa michepuko yake.
16. Ni aibu na fedheha kumbembeleza mwanamke anayejua kuwa anakukosea kwa makusudi.
17. Ni aibu na fedheha kumaliza makanisa ukiwahadithia wachungaji tabia mbaya na usaliti wa mkeo.
18. Ni aibu na fedheha mkeo kukunyima unyumba ukaenda kumshitaki kwa wazazi wake wakati unajua cha kufanya.
19. Ni aibu na fedheha v mara kukopakopa kwa wakwe zako tena waliostaafu kazi..ni aibu ni aibu kubwa.;
20. Ni aibuu na fedheha kwenda baa na mke baa au sehemu za starehe kila siku ikija bili unapewa wewe nawe unampa mkeo alipe kazi kukuna tu kidevu na kwenye wallet umejaza business card na viwembe vya kugushi nyaraka mitaani.

Hizo ni baadhi tu ya aibu za wanaume waliowengi karne ya leo. Sambasa wajijue na wamuombe Mungu awafungulie milango nao wawe wanaume katika nyumba zao.

AINA KUMI ZA NDOA HIZI HAPA.

Leo hii tutaona aina kumi za ndoa kama ifuatavyo:

1. NDOA YA MKEKA
Inatokana na kufumaniwa na Binti wa watu.Ndoa hii huwa Haina mahari. Hii huvunjika mwaka mmoja tu,baada ya wanandoa kugundua hawakuwa wakipendana!Ni maarufu sana kwenye miji ya Pwani san asana uswahilini.

2. NDOA YA MIHEMKO (NYEGE)
Hufungwa na vijana wa kiume  wenye umri wa miaka kati mume 22 mpaka 25  na  mke miaka 19 mpaka 23.Mara nyingi vikao vya harusi uanza pindi kijana anapokuwa amepata kazi baada ya kumaliza elimu ya chuo na uvunjika baada ya miaka 2 au 3 ya ndoa,kwani wanandoa wanakua sio wakomavu(mambo mengi ya mihemko kama vile kuchepuka nje ya ndooa wanakuwa hawana uzowefu nayo).

4. NDOA YA MAONYESHO
Wenye ndoa hii hupenda kujionyesha barabarani na mara nyngi wanandoa hasahasa wanawake ufose kingi aolewe kwa ajili ya mashindano tu na shoga yake kwasababu nao wameolewa basi nayeyey lazima aolewe tu ili kuondoa mkosi tu,na mara nyingi ndoa inakuwa ni ya ukumbini tu lakini rohoni hamna kitu.Ila ndani hazina utii.Hupigana kila wanaporudi kutoka kwenye mizunguko. Cha kushangaza huwa hazivunjiki lakini ndiyo ndoa zinazoongoza kwa kuchepuka!

5. NDOA YA UHAMISHO.
Hufungwa na watumishi wa vijijini na mjini. Ili wa kijijini ahamie mjini.Mahari utoa anaetaka kuhamia mjini. Hata kama mahari atatoa mume lakini hii ndiyo ndoa yenye ukakasi zaidi.Huvunjika mara tu wanapoanza kuishi wote mjini. Salama ya hii ndoa ni kuhama kutoka mjini kwenda kijijini.

6. NDOA YA MIMBA.
Hufungwa kwa sababu wanaoowana hawataki kuonekana makwao kuwa wamezaa nje. Au muolewaji alikuwa hampendi muoaji kwa dhati.Mara nyingi muolewaji hutumia mimba kama mtego wa kuingia ndoani. Hii huvunjika mtoto akizaliwa na kufikisha mwaka 1 au 2.Mara nyingi utengenezwa na mabinti wa mjini hasahasa wasomi   au wenye kipato na kazi nzuri.Hapa mara nyingi muolewaji anakua ameshapata kila kitu katika maisha kasoro mume tu!

7. NDOA YA MALI (UTAJIRI)
Muolewaji miaka 18 au 28 Muoaji 65 au 70.Ndoa hii pia huitwa ndoa ya babu na mjuukuu. Ndoa ya aina hii hudumu, kwasababu mwenye kauli ni mwenye mali. Asilimia kubwa ya waume wa ndoa hizi hulea watoto wasio wao.

8. NDOA YA KWASABABU.
Hufungwa ili mradi muoaji au muolewaji aonekane tu kwa jamii kuwa naye kaoa au kaolewa.Huwa hazina utii wala upendo dhati. Ndoa ya aina hii ikifikisha miaka 4 huwa hazivunjiki wahusika huishi kwa ajili ya mazoea na watoto.

9. NDOA YA UPENDO.
Ndoa hizi ziliishia mwaka 1978 kabla ya vita vya kagera.Muoaji na muolewaji hawakuangalia vitu ila utu tu ambao uliwaunganisha na kutengeneza upendo wa kudumu. Hii ilidumu miaka yote.

10. NDOA KUCHUMA

Ndoa hii ufungwa ili mradi muoaji au muolewaji akapate kitu au vitu Fulani(kama vile kazi,mali,umarufu,tenda) kutoka kwa mpenzi wake au wakwe upande upande wa pili . Hii hudumu miaka kadhaa kutegemea na malengo ya mhusika. Wengine husubiri mpaka mhusika afe,lakini hujikuta wanakufa wao kwanza.