Jumanne, 3 Mei 2016

WASIMAMIZI MSETO WA NDOA KUPEANA NAMBA!

  1. Nimejaribu kuangalia baadhi ya wanandoa mbalimbali na kuona kuna mengi sana yanayotokea hivi sasa
    naomba nieleweke sikutishi uoe ama kuolewa ila vyema kujua ndoa sio lelemama na unapoamua kuingia usitarajie msaada wa mamako ama babako.

    Ataa wanakula kiyoyozi ukahisi wako peponi kumbe mmoja wao anatukana kisisiri huyu polisi vipi anatuchelewesha nikammwage huyu nianze zangu.....sitaki ufanye hivi nasema kwa kukuonya muwe makini sana na ndoa tunazofunga

    Usifunge ndoa kwa ajili ya shangazi ama mjomba ama baba ama mama utalia..wengi wameingia kwenye sumu hii na kuishia kugawana pepo walizocchuma wakiwa duniani baada ya miaka kadhaa..mbaya zaidi hivi sasa unakuta babu na mvi zake ati anaenda mahakamani kuomba bibi ampe talaka laana ilioje...

    So ni kweli ukiwa single unakuwa na furaha ya kujiamulia mambo na kufrahi kwenda unapotaka lakini ukifika kwenye ndoa ndugu ujue kuna serikali ya NDOA..na mawaziri makatibu manaibu na diwani pamoja na wabunge woote ni wewe na mkeo na majukumu yote mwaitaji kuyafanikisha pamoja ili msikae vikao vya kusuluhishana....

    Mwisho nawatakia heri na fanaka kubwaaaa kwa wapendwa wetu walioamua kufunga ndoa Kanisani/MSIKITINI/BOMANI na sehemu mbalimbali maana nimesikia mbeya huko kuna wachungaji wanawawafwata wanandoa nyumbani na kuozesha..si haba hali wamependana...nawatakia harufu njema ya amani upendo na mzidi kuongeza dunia kama wazazi wenu wasivyokuwa wachoyo kuwaleta nyie dunian leo hii mnafunga ndoa......

    WASIMAMIZI

    Siku hizi kumekua na katabia ka kusimamia ndoa wasimamizi mseto!....yaani hili ni balaa jingine!Tafadhali ukiwa unatarajia kusimamia ndoa ya mtu jumamosi ijayo ama ijumaa mkiwa kama wasimamizi mseto jamani punguzeni ukaribu...sie wake zetu tunawaruhusu kwa kuwaheshimu wanandoa lakini naona hivi sasa mtu yuko mbele anajiachia uku akikumbatiwa na msimamizi mseto wakipeana namba fasta kwenye hai tebo baada ya hapo ni chating tu!....."baby ulikua wapi nilitakiwa nikuoe wewe  angalia jinsi ulivyojazia!"

    Hili tusingependa litokee kama si mkeo lishaneni keki mshibe muondoke si mambo ya umependeza oohh unajua angechelewa walahi ningekuwa na wewe toka hapa ulikuwa wapi siku zote!Itafika wakati inabidi wake zetu wakisimamia ndoa tuende na panga kwenye makoti yetu meusi kuleta heshima kwa wasimamizi hilo ni wazo...karibia na utani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni