Jumatano, 19 Oktoba 2016

NDOA ZA SIKU HIZI UTASIKIA...WAMEACHANA!

Vijana wengi wanatamani kuoa na wasichana wengi wanatamani kuolewa. Mimi ni miongoni mwa vijana wanaojiandaa kuoa na hivyo niko katika kipindi cha kuyatafakari maisha ya ndoa.

Jambo moja ambalo limenishangaza ni wimbi la kuachana wanandoa. Asilimia kubwa ya marafiki na jamaa zangu walionitangulia kwenye ndoa hawako pamoja leo hii. Siyo wadada wala wakaka ukija kusikia eti walishaachana. Tena wapo waliokuwa wanapendana sana kiasi kwamba niliamini ni kifo tu kingewatenganisha lakini leo hii nasikitika kusikia wameachana.

Tatizo ni nini wakuu? Zamani watu walikuwa wanaachana lakini siyo sana kama siku hizi make ilikuwa ni aibu kuachika na baadhi ya makabila mtoto wa kike alikuwa anaambiwa akiachika asirudi tena kwao, kwa lengo la kumfanya aiheshimu ndoa yake na awe mvumilivu.

Baadhi ya watu wazima wameniambia kuna tatizo la feminism, wanawake wengi hasa wenye vipato wanapenda kushindana na wanaume hawajishushi kama wanawake wazamani ambao hata wakipigwa walikuwa wanavumilia tu.

Pia michepuko ya wanaume ni tangu zamani lakini siku hizi mwanaume akichepuka na mwanamke naye anataka kuchepuka ili alipize mwishoe ni kuachana tu.

Kingine watu wamepungukiwa na uvumilivu, juzi nimepigana sana kuokoa ndoa ya mdogo wangu ambaye alitaka kumuacha mkewe waliyezaa naye watoto wawili ili aoe kabinti ka Chuo Kikuu bila sababu zinazoeleweka lakini mwishoe nikabaini huyu amemchoka shemeji tu. Wanawake nao mwanaume akichoka mathalani hana hela tena au kaishiwa nguvu za kiume wanaanza visa mwishoe wanakimbia.

Nini sababu nyingine zinachangia? Karibu mtoe maoni tuwaandae vijana kabla hawajaingia kwenye ndoa takatifu.


Joyce:
Binafsi i don't believe in marriage japo nipo kwenye ndoa ila anytime ntaiacha maana ninayokutana nayo ni makubwa na si swala la uvumilivu no mimi nimevumilia kwa miaka minne unaenda wa tano ila mtu ndo kama anakuona unajipendekeza na huna pa kwenda, nadhani kiburi cha pesa na hulka ya mtu binafsi kuwa na wanawake wengi pia vinachangia ndoa nyingi kuvunjika,mwanamke unaweza ukavumilia na kujaribu kumrekebisha ila mwanaume anakuona km unampanda kichwani na kumfatilia mambo yake so hapo ndo kuna tatizo

Aron :Binafisi nikweli ndoa za zamani zili dumu nikisema mazingira ya kipindi iko yali luhusu,unakuta mwanamke tangu aolewe anashikwa kiuno na mmewe pekee ila nambie saivi hali ilivo.kwa wanaume sasa ndio usiseme.Kipindi iki ndoa zina changamoto kupita kiasi.

Kiukweli tuache kufalijiana ndoa za kweli ndio zinaishia.

Wanao sema ndoa raha waulize wamepitia matatizo mangapi bado wakaiona ndoa ni raha.

Kwa ufupi naamini miaka ijayo mtu mwenye akili timamu(ukiacha hawa wanao funga ndoa kuepuka dhambi ya zinaa) atakae kua kwenye ndoa atashangaza sana.



1.    NDOA za siku hiz tunavumiliana tuu tukichokana Tuna Achana Ndoa zilukuwa zile za Ma Babu zetu na Bibi zetu sio hiz za kuoa au kuolewa kama fashion tuu
Ndoa ni tendo la kiimani hivyo wanandoa inawapasa kumtanguliza Mungu mbele ili aweze kuilinda ndoa yao. Vijana wa siku hizi wakimaliza kuoana hawamuhusishi tena Mungu wao,, Hawaendi Misikitini wala Makanisani. Hawasali pamaoja! Sala ndio nguzo pekee ya ndoa! Muwekeni Mungu wenu mbele nanyi mtaishi miaka mingi kwa raha daima!


Pia vijana waache kuhusisha maisha ya ndoa na mambo ya social networks.. Social networks ndio chanzo kikubwa cha kuvuruga ndoa nyingi! Wana ndoa wanapotaka kuiga mambo ya watu wengine wanayoyaona kwenye social network ndio tatizo linapoanzia hapo. Mdada anaona mwenzake kila siku katolewa outing na mumewe naye anataka mumewe amfanyie vivyo hivyo bila kujali mpangilio wao wa kimaisha yeye na mwenza wake!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni