Wadau kuna mdada
mmoja mrembo ambaye ni mtoto wa mjomba, ni mwezi mmoja sasa tangu
tumefahamiana.Mwanzoni tulipokutana, alikuwa ananiita kaka, Mara akaanza
kujiita mke mdogo, lakini sasa siku zinavyozidi kwenda ananiita baby.
Nisipowasiliana naye siku mbili tu analalamika nimemtenga, siku akiwa off
anataka niende kwake nikamtembelee.
Nakumbuka alilalamika sana kwanini sijamnunulia nguo za
sikukuu ya EID, akadai nampendelea sana mke mkubwa tu, yaani mke wangu wa
ndoa.Jamani hivi maisha ya ubinamu ndio yako hivi?
Denis:Kuna usemi unasema "Binamu nyama ya hamu".
Labda binamu anataka kuprove kama ni kweli au ni usemi tu.
Clara :Ma Cousin ni changamoto kweli kweli, mpotezee tu!
Benard: Mkuu, heshimu ndoa yako.. heshimu mke uliyemtukuza
kuwa mama watoto wako.. "Utanusurika ukijinusuru!!"
Huyo binamu mnunulie zawadi akitakacho halafu mpe wife
(mkeo) ampe kama zawadi... ila hizi tabia za baadhi za uswahilini huharibu
nyumba nyingi na kusamabaratisha familya!!
usifunguwe mlango wa nuksi....
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni