MKE WA MTU SUMU AU SUKARI?
Kama mjuavyo mitaani kwetu mara nyingi watu mnakuwa mnajuana, Yule fulani
anatoka na fulani, sasa basi kuna jamaa yetu bwana alikuwa anamgonga mke wa
mtukwa mda mrefu sana na watu kitaani tulikuwa tunajua, mshikaji alikuwa na age
kama ya miaka 28 hivi na huyo demu alikuwa same age na jamaa.
Basi bwana
mshikaji akawa anajigongea kama kaoa vile, mahaba yakanoga nakama mjuavyo mahaba
yakinoga lazima mtajisahau, yakanoga ile mbaya kiasi kwamba mshikaji akawa
anapikiwa msosi home kwa dem anapelekewa geto kwa mchizi.
Yakaendelea
kunoga zaidi na zaidi mchizi alikuwa anamtoto alizaa na dem mwingine
akawaanampeleka kushinda na yule dem siku nzima.
Wakati yanafanyika haya
yote mume wa yule dem alikuwa anaona na anajua ila aliuchuna kama hajui lolote
ila ukweli ni kwamba alikuwa anajua kila kitu.
Kama mjuavyo washikaji
sometimes mkikaa nyumbani huwa mnapiga story zinazowahusu, kuna siku bwana
niliimuuliza mchizi kuhusu mahusiano yake na yule dem (mke wa mtu) mume wake
anayachukuliaje ukizingatia jamaa anajua kila kitu.
Jamaa alichonijibu
akasema jamaa (mume wa mtu) haongei kitu kwa mkewe kwasababu mkewe kamtengeneza
vyakutosha, (muvi hili lilianza kama miaka miwili nyuma).
Basi bwana,
muvi lilianza kunoga zaidi siku nne tano zilizoisha yule dem(mke wa mtu) alibeba
ujauzito wa mchiz na mimba ilikuwa kubwa tu ya miezi kama sita hivi, kukatokea
kutoelewana kati ya mchiz na yule dem.
Yule dem akaamua kuitoa ile
mimba, kile kitendo cha yule dem kuitoa ile mimba mchiz kikamkera sana, akamwita
dem geto kwake kichapo alichompa nusu amtoe roho kama sio majirani kuvunja
mlango kumuokoa yule dem.
Dem kurudi kwake mumewe anamuona na majeraha,
kuuliza vipi mkewe anajiumauma jamaa akajua aliyefanya hivi atakuwa
mchiz.
Akamfata mchizi geto kwake akamwambia sasa wangu ulipofikia hapo
sipo,akamwambia mimi sio mjinga kama mke wangu alivyokwambia kwamba
amenitengeneza hivyo siongei kitu.
Ukweli ni kwamba mimi na mke wangu ni
waathirika wa HIV kitambo sana ndio maana sikuwa na wasiwasi wala presha ya
kukimbizana na wewe.
Kama uliamua kutembea na mke wangu sio mbaya ila
mambo ya kunipigia mke wangu mimi siyataki. Jamaa akamaliza kuongea akasepa
zake.
Baada ya jamaa kumfata mchiz na kumchana, jumatatu ya wiki hii
akaenda kupima HIV bahati mbaya kweli akakutwa ameathirika.
Basi kurudi
home mchizi akaamua anywe sumu, (hapa nawaunganishia matukio ili mpate mtiririko
mzuri, kwasababu sisiwenyewe tumejua yote haya baada ya jamaa kuacha ujumbe
baada ya kujiua).
Basi mchizi jumatatu (ya wiki hii) hajatokea skani,
jumanne (juzi) akaja ila hakuwa yule tunayemjua, hakukaa sana
akasepa.
Jana nipo job mida ya tisa hivi napigiwa simu naambiwa mchizi
amekunywa sumu, amegundulika kama amekunywa sumu baada ya majirani kumsikia
anakoroma ile mbaya.
Kuvunja mlango kuingia ndani wanamkuta jicho
lishamtoka yupo kwenye hatua za mwisho,wakajaribu kumywesha maziwa ikashindika,
wakambeba mpaka hospital wakamchomasindano mbili na dripu.
Wakaambiwa
wampeleke Lugalo kufika Lugalo wanaanza kumpa huduma mchiz akakata roho. Mchizi
aliacha barua akaelezea sababu ya kuchukua maamuzi hayo mazito.
Kubwa ni
hilo la HIV, mchizi tumemzika leo mida ya saa 10. Hili ni tukio la pili sasa la
kwanza lilitokea miezi kama mitatu au minne hivi iliyopita baada ya mjukuu wa
mzee ruksa kujiua kisa kikiwa cha mapenzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni