Huyu mkeni mrembo nilimuoa akiwa hana kitu, kwa bahati
alitafutiwa kazi na ndugu yake kwenye kampuni moja ya simu akawa analipwa kama
milioni 3 kwa mwezi fasheni na yeye yeye na fasheni vipodozi kila aina,handbag
na nywele za laki tatu ndio mshahara wake ukawa unaishia huko mimi mshahara
wangu hauzidi laki sita,nilifanyishwa vituko vyote ndani ya nyumba ,manyanyaso
yote ,hapiki hafui,hafanyi chochote ndoa ikawa inaelekea kuvunjika.
Nikaenda mahakamani kuprocess talaka wakasema mpaka nianzie
baraza la usuluhishi la kata au kanisani,nikaamua kwenda kanisa tulilofungia
ndoa tukaitwa kwa Baba Paroko for hearing sijui mediation sijui arbitration
sijui mie nikatinga kwa bajaj ya kukodi nimepaukaaa yeye akaja na RAV4 .
Baba Paroko alivyotusikiliza akaaniita pembeni akasema
kijana hapa nadhani hata tukiomba na kukariri mistari yote ya biblia plus
mapambio yote ndoa yako haitarudi kama mwanzo pambana utafute hela tu.
Nilisali sana nikasugua goti nikamuomba Mungu baada ya miezi
mitatu hivi mambo yangu yakakaa sawa mshahara ukawa mara mbili plus marupurupu.
Siku moja mara ghafla simu yangu inaita ni mke wangu sikuhamini
kwani huwa hanipigii mpk jioni tunakutana nyumbani nilishangaa mke wangu
kunipigia mchana ,ooooh mume wangu tumeachishwa kazi kampuni imeuzwa,hureeeeee
niliruka ruka kwa furaha sana nikapigia simu washikaji tukaenda kunywa bia na
nyama choma mpaka saa sita usiku kabla polisi na makonda hawajatuvamia nilijua
ile kazi ndio inaniharibia ndoa na aliipata kibahati hawezi tena kupata kazi
kama ile.
Hela yote ya NSSF akajaribu kufanya kila biashara biashara
zikabuma mtaji ukakata alijifanya hajui kupika sasa anapika kuliko hata wapishi
wa Kempinski, alijifanya sijui hawezi kufua sasa anafua kuliko dobi ,kitandani
alijifanya mvivu sasa yuko vizuri kuliko wacheza shoo wa fally ipupa, RAV4
imepaki tu muda wote ananilelea watoto kwa nini nisimshukuru Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni