SIMU YA MKE WANGU
Ni hivi mimi nipo Dsm na mke wangu yupo korogwe Tanga.
Tulikuwa tunaishi
wote hapa Dsm kabla hajapata kazi kisha akapata kazi na kuelekea
huko.
Kabla hajaelekea huko Tanga hapa jirani kuna baba mmoja ni mlokole
anavojiweka mwenywewe na ana mke na watoto wakubwa wa kwanza yupo
chuo.
Tulivyoishi
Huyu jamaa akawa yupo jiran na mke wangu, yan
kumpigia simu na kushauriana mambo kadha wa kadha hasa ya kanisa kwa vile
nilimwamini mke wangu sikuwa na wasi wasi...na kikubwa zaidi akawa anampigia
wakati wowote akiwa na suala hasa kikanisa...
ikafika stage wife akaondoka
akaenda kikazi tanga...
akiwa tanga nilinunua smart phone na
kumpelekea....
kwenye ile smart phone nikaweka program ya kunitumia taarifa
zake ikiwemo msg na calls zote ziingiazo na kutoka kwenye ile
simu...
Ilivyoanza
Huyu jamaa alikuwa anajifanya mpole na
kuhitaj kuwa karibu na kumchukulia kama family friends....yan familia yangu
ikiwa na shida gari lake linatumika na familia yake ikiwa na shida kama
wakilihitaj gari linatumika.
Tukiwa pamoja na huyu jamaa namheshimu sana
as family friend na naye akawa anaonyesha heshima ya juu sana nikamuona ni mtu
mwema kwa kizazi na maisha ya watu leo kumbe anakuja kunitenda kwa kutembea na
mke wangu na kuniachia kovu ambalo sijawahi kuhisi maumivu yake.
Ni bora
utendwe na mtu alie mbali nawe kuliko yule uliemwamini na kumheshim sana halafu
anakuja kumvua mkeo chupi, hiki ndo nikikumbuka nalia kidume mimi.
Hapa
nitaeleza dalili za mwanzo kati na hadi mwisho wa kuja kukamatwa kwa huyu
alieniliza kidume mimi.
Lengo la hii thread nitaomba ushauri wenu
nitarudije normal na pia nimfanyeje hawa wezi wote mke na mme.
Nilivyompa
ile simu ikiwa tayari ina hiyo application nikalala asubuhi yake nikaondoka
kurudi DSM
ile nipo kwenye dar express mida ya saa tano nikaletewa
notification kwamba kuna mu anangea na wife.
Kucheki namba ni jirani
yangu, nikapotezea nikaendelea na mambo mengine mida ya saa saba mchana
notification simu inatumika kucheki ni jamaa jirani, saa kumi notification
kucheki ni jamaa saa kumi na mbili notification kucheki ni jamaa saa moja na saa
mbili notification kucheki ni jamaa tu.
Machale yakanikuna kuwa kuna kitu
hapa.
Asubuhi yake mapema jamaa kampigia tena ilipofika saa 4 wife
alienda church kwa hiyo alikuwa amezima simu jamaa kamwandikia messge mbona
hupatikan nimekumiss sana.
Hapo alarm ya kichwa ikapiga kwamba kuna jambo sio
dogo hapa.
Ile wife ametoka kanisani akawasha simu basi muda huo huo
nikaletewa notification kwamba jamaa anaongea na wife.
Walivomaliza
kuongea wife akanipigia simu akanipa hai tukaagana akakata simu.
Baada ya
kukata simu wakapigiana tena na tena yani jamaa anampigia wife kila baada ya saa
moja au mbili.
*Baelezee*
Tulivyoishi
Huyu jamaa
akawa yupo jiran na mke wangu, yan kumpigia simu na kushauriana mambo kadha wa
kadha hasa ya kanisa kwa vile nilimwamin mke wangu sikuwa na wasi wasi...na
kikubwa zaidi akawa anqmpigia wakat wowote akiwa na suala hasa
kikanisa...
ikafika stage wife akaondoka akaenda kikazi tanga...
akiwa
tanga nilinunua smart phone na kumpelekea....
kwenye ile smart phone nikaweka
program ya kunitumia taarifa zake ikiwemo msg na calls zote ziingiazo na kutoka
kwenye ile simu...
hapa mwanaume nimeamua kuweka ukweli wangu kama
yamenikuta yaweza kukuta na ww naomba mzahamzaha sipendezwi
wakuu
*************
basi vile nilivokuwa napata zile notifications
mara kwa mara za meseji na calls kwa jamaa kwenda kwa mke wangu nikashindwa
kuvumilia ikanibidi niende korogwe kwa wife...nikampigia simu kwamba nakuja
tanga, wakati nakata simu ikaingia notification kwamba jamaa anaongea na wife
kumbe wakatumia wakati huu kuambizana kwamba nipo njiani naekekea tanga, hivo
zile notification za mawasiliano yao zikapungua kuja kwangu....
Nimefika
tanga nikamkuta wife yupo normal tu na simu yake ipo loose tu juu ya
meza....basi akanipokea pale kwa bashasha yani full tabasamu (dont trust a
woman) akaandaa chakula tukala tukalala....
usiku mida ya saa 3 usiku
ikaingia txt kwenye simu yangu nikaichukua ile msg nikaisoma ilikuwa ya kikazi
nilivomaliza kuisoma nikairudisha simu kwenye dressing table...hapo nikaona wife
amenyanyua kichwa akaniuliza msg ya nan nikamjib ya kazini akanyanyuka kuichukua
simu yangu nikaidaka na kukataa aiguse sababu kubwa nina hasira za kimia kimia
moyoni kwamba najua nn kinaendelea ila najipa muda. .akanituhumu pale kwamba msg
ya mwaamke ndo maana nakatalia aione.
akanijibu jibu moja kwamba mm sio
mwaminifu ndo maana nakatalia simu akadai kwamba mbona yeye simu yake ipo free
na kama nataka nikae nayo hata siku nzima hamna kibaya kitakachoingia (hili jibu
hutolewaga na wasichana na nilitumia kuliamini sana kumbe sio) kuweni makini
utakaa na simu ya mkeo au mchumba na still akakucheat....basi tukakwaruzana pale
kidogo kisha tukalala.
asubuh nikaamka nikarejea dsm
hii
siku nzima ilipita sikupata notification ya mawasiano yao.
kesho kutwa yake
nikaendelea kupata notification za mara kwa mara kwamba wanaongea na msg za hapa
na pale yaani wanaongea hadi saa 4 usiku sometime.
nikashndwa uzalendo
nikaanza michakato kila anapomaliza kuongea nampigia simu namuuliza ulikuwa
unaongea na nani akawa anataja ndugu zake na anakupa hata sababu walichokuwa
wanajadili.....nikawa namkubalia kwa shingo upande kwan notification za txt zote
na calls zote anazopata nazipata..
ipo siku tena nikaamuliza akawa mkali sana
kwamba iweje anipe taarifa za kila anaempigia je mbona mm simpi.
nakumbuka
ilikuwa jumatano nikaletewa txt as notification toka kwa jamaa anamtaka wakutane
ijumaa wasex.....jamani jamani jamaniiiiiii inauma asikuambie mtu.....nilivuja
jasho sijapata kuona nikakabwa na kitu kooni nikavumilia.
wife akamjibu sawa
karibu hata mm nimemiss mambo yako...
.hiii jumatano sikulala kabisaa
kwan walizidisha muda wa kuongea walichati sana msg za kawaida na
kijinga......kipindi hiki wanaendelea wife alikuwa ananipigia sim kama kawaida
tunaongea ila alinote sipo sawa akaniuliza kuna nn nikamjib hamna
shida...niliamua kuondoka dar saa 11 jioni alhamisi kwenda korogwe ili kuliwah
siku ya tukio yani ijumaa wanapokutana.
nimefika korogwe ilikuwa kama saa 3
usiku niliwaza sana kabla sijaenda nyumbani kwa wife
niliwaza nijifiche ili
kesho niwakamate
niliwaza je nikiwakamata kesho nn kitatokea
niliona jibu
lepesi ni kuwaua wote
*******************************
hiyo alihamisi
jioni nikakodi chumba korogwe nilale...ila usiku saa 4 hivi nikahisi sipo sawa
kabisaa kila kitu nakiona kichungu..
nikawaza bunduki sina, panga sina, je
hawa hiyo kesho nitawauaje? je wakishaingia gest mi nae nikaingia afu nikakute
wamemaliza kufunga mlango itakuaje? je zikianza purukushani za kutaka kubomoa
mlango na mhudumu akawaomba watu msaada kwa kupiga kelele si watanishika na
jamaa atakimbia..
m
niliwaza sana pale gest nikiwa kitandani, wazo
likanijia kwamba sitapata hata tone la usingizi pale ni bora nimfuate wife
nianze nae kwanza kupata ukweli...ile saa tano usiku nikapata tena notification
wanaongea hasira zikazidi nikaamka kumfuata nyumbani kwake hapo korogwe saa 6
usiku nagonga kwa wife na inaonekana alikuwa hajalala..
Nilipofika kwa wife
kwanza alishangaa iweje umekuja usiku hivi...nikamwambia nilikumiss na
ni suprise yangu kwako.....nikajikaza sana kidume nisioneshe
hasira.
Matukio
Nilipofika ndani nikakaa kitandani nikavua
viatu na soksi nikapanda kitandani sikuvua suruali wala shati coz nilijua
hapatalalika,
cha kwanza wife akaonyesha kuhamaki kidigo afu akapotezea
simu yake ilikuwa juu ya dressing table tena kwenye chaji kabla hajaenda
kuniandalia maji ya kuoga bafuni nikaona anaichomoa kwenye chaji na kuihamishia
kwenye begi la nguo juu lilikuwa mwisho wa kitanda upande wa
pili....
nikaamuliza mbona unatoa simu chaji akajibu imejaa..
nikamuuliza
mbona unaihamisha akajib nimeweka vibrate kwa hiyo hapo inaweza vibrate
ikakudisturble na pia ikadondoka.
nikamwambia wakat unaenda kuniandalia maji
naomba niicheze chezee hapa hizo games zake.
akanipa ila hana aman akaelekea
bafuni.
Kwenye Simu cha kwanza nilicheki txt zote zimefutwa japo mm
ninazo kwenye simu yangu.
cha pili calls zote zinafutwa akishamaliza kuongea
nae hivo kwenye simu yake hakuna evidence yoyote japo mm ninazo kwenye simu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni