TUNZA SIRI ZA MWENZANKO BASI
Weekend hii bhana nilienda kumtembelea best angu mmoja hivi sasa katika
tembeatembea tukakutana na mbaba mmoja hivi jirani ake, baada ya salamu akapita
zake best akaniambia namuonea huruma kweli huyu baba siku atakapogundua tabia ya
mkewe sijui itakuaje,
Ni hivi huyu mke wa huyu jamaa ana tabia ya
kusimulia madhaifu ya Mme wake kwa mashoga zake anadai kuna siku moja huyo
mwanamke alikuwa anawasimulia;
''Yaani huyu mwanaume natamani nimuache
hata leo kitandani hawezi chochote yani kinachonifanya niendelee kuishi naye ni
kwa vile ananijali na ananipa kila nachotaka lakini kwenye swala la 6/6 ni sawa
na ananichafua tu. Ila nina mtu ambae ananifikisha ninavyotaka''.
Wakati
anaawaambia hayo mara akapigiwa simu na mume wake basi akawaambia ''ngoja niende
huyu ----- ananiita naona anaongea kwa ukali kweli sijui kapatwa na
nini''.
Anavyodai alivyofika kwake huko kamkuta mmewe kafura hatari kabla
hajakaa kapokelewa na kibao hajakaa sawa kingine ''nini mume wangu mbona
unanipiga nimefanya nini?''. Mume wake kwa hasira, ''nimekusikia yote uliyokuwa
unawaambia mashoga zako''.
Mwanamke akaachia kicheko akamwambia, ''Mume
wangu hicho ndo kinakufanya unipige me pale nilikuwa najaribu kukulinda mme
wangu kuna shoga angu mmoja nasikia anakutaka na anasema atafanya chochote il
aweze kukupata, kwa hiyo nilifanya vile ili kumkatisha tamaa si unajua
ninavokupenda Mme wangu''.
Basi mwanaume akanywea akasema, ''basi
samahani mke wang nilifikri una mtu mwingine zaidi angu'' mwanamke tena akamjibu
''ninavokupenda mme wangu njoo unipe haki Yang kwanza''.
Basi
walivyomaliza mchezo wao mwanaume akapitiwa usingizi, yule mwanamke kaenda
kuwasimulia mashoga zake kila kilichoendelea alivyomaliza akawaambia ngoja
nirudi asije akaamka akanikosa.
Wakati anaudi kwake shoga ake mmoja
akachukua simu akampigia simu akamwambia tunajua kila mlichokifanya mkeo kaja
kutuambia mwanaume alichojibu huyu mwanamke vipi anatoka nje harakaharaka
anakutana na kutana na mkewe mlangoni katoka kuoga kamuuliza unatoka wapi
alichojibu ''mme Wangu si unaona nimetoka bafuni kuoga baada ya shuhuli pevu
ulionipa?".
Basi mwanaume hakuwa na la kufanya zaidi ya kufikiria kuna
watu wanataka kuwachonganisha.
Mimi kwa upande Wangu sikufurahishwa na
tabia ya huyu mwanamke, hamtendei mwenzie haki hata kama ana mapungufu hakupaswa
kumuacha mwenzie uchi hivi. Sijui ingekuwa ni wewe ungefanyaje?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni