Sijui ni masifa au nini ila kwa kweli sio vyema kabisa
unamkuta mdada kavaa nguo ndefu tu ila tatizo ni transparent zinaonyesha hadi
chupi na sehemu nyingine za maungo yao kweli sio vizuri wanaume tunapata wakati
mgumu sana kwani nguo zenu zinatuhamasisha kufanya ngono na vitendo vingine vya
kichochezi.
Ni hali ngumu sana unapokatiza
mjini/mtaani/shule/vyuoni/daladala unakutana na haya maafa kwa kweli wanawake
mnatumaliza sisi wanaume.Nidhamu ya mavazi ichukue mkondo mavazi yenye
kuonyesha sehemu za ndani yaachwe pia nguo zinazobana zinaonyesha hadi mistari
ya chupi ziachwe nasema tena maana hamna namna hata hizi fupi zinazoonyesha
mapaja na viuno mziache mwanamke vaa vazi kubwa la kufunika na kusitiri mwili
wako wote.
Mi langu rohoni leo nalitua,ukweli nakereka na kujiskia aibu
kwa hili.Yani unakuta mdada au hata mwanamke mtu mzima anafanya makusudi
kuingia kwenye shughuli za watu za heshima zinazohitaji mavazi ya kujisitir
angalau basi nguo iishie magotini na kuficha sehemu nyeti na kama matiti na
mapaja...
Ye utakuta kaingia na kigauni utadhani cha mtoto wa shule ya
msingi miziwa yote ipo nje nje..Mipaja yake nusu na robo ipo nje,sasa hapo hata
akiangusha kitu sidhan kama ataweza okota!Alafu kihelehele uyoooo anaomba asevu
high tabo!
Sasa hebu fikiria watu wanafanya shughuli ya kumuaga binti
yao (send off) au harusi ukumbini..kule mbele kuna wazaz na wazee wetu wengine
wa heshima,upande mwingne wamekaa wakwe..
Muda wa kucheza mziki unaingia pale mbele kwa mbwembwe zote
shost unajimwaga ukiwa nusu uchi na kutuaibisha wanawake wenzio hadi tunaona
aibu,mi nlishuhudia zaidi ya sherehe moja..
Tena mdada anawapa mgongo wazazi wa yule shogake anayeagwa
uchezaji wenyewe wa kujibinua ka' mbuzi anetolewa kafara,huku nyuma mipaja yote
nje bado sentimeta moja matako yaonekane,mama mzaz akainamisha kichwa pale kwa
aibu ya anachoona.
Mi nnachoomba angalia dressing code yako kwa eneo husika,sio
unavaa mradi kiende.Utavaaje kigauni cha klabu kwenye wedding reception zetu za
kitanzania? halafu ukiangalia nyomi lote walovivaa unakuta ni ww au kuna
mwingne pemben ndo mlovaa kiaibu tu..
Hata kama ni kwenda na fashion zingatien mahali mnakoenda
hata kama hakuna wazaz au wazee wenu bado waliopo watawachukulia kivingine tu!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni