Ijumaa, 24 Juni 2016

WADADA WAZURI PUNGUZENI NYODO

Nakumbuka kuna siku nilikua nimekaa maeneo ya Mwenge naosha miguu kuna mdada duu nae akaja mzuri hatari t#ko kubwa full nyodo tuuu hatari hakusalimia wala nini akauliza tu kaka utatumia muda gani kummalizia huyu mdada?Akajibiwa pale akatulia akawa anachat na Galaxy baby mi nikamsalimia (kwasababu nilitaka kujua handbag yake amenunua wapi imekaa kiulaya ulaya na vitu alivyotupia kwa jicho la haraka unaona vimeshuka na ndege).
Bidada alininyali mpaka nikatamani Dunia ipasuke,tukaendelea kukaa alikua amevaa kimini cha rangi ya cream  na top nyekundu.Muda si mrefu si bleeding iyoooo!ikampata ana hahahaaaa utadhani nguruwe anataka kupandwa mi nikawa namwangalia tuu!
Tone jekundu hilo mmmh! nikaingiwa na imani kwa kweli maana hiyo sehemu wanaume kibao nao wapo ambao ni wasusi nikaona tutasemwa wanawake wote na sio yeye nikaingia kwenye mkoba nikampa mtandio na kumrushia mineno ya shombo akuamini mara dada naomba namba zako ili nikurudishie mtandio wako nikamwambia nim,ekupa bure !Yaani nikikutana nae barabarani full kujichekesha kwangu ,nimemdharau sana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni