Jumanne, 2 Agosti 2016

BINAMU ANAPOANZA KUKUITA BABY!

 Wadau kuna mdada mmoja mrembo ambaye ni mtoto wa mjomba, ni mwezi mmoja sasa tangu tumefahamiana.Mwanzoni tulipokutana, alikuwa ananiita kaka, Mara akaanza kujiita mke mdogo, lakini sasa siku zinavyozidi kwenda ananiita baby. Nisipowasiliana naye siku mbili tu analalamika nimemtenga, siku akiwa off anataka niende kwake nikamtembelee.

Nakumbuka alilalamika sana kwanini sijamnunulia nguo za sikukuu ya EID, akadai nampendelea sana mke mkubwa tu, yaani mke wangu wa ndoa.Jamani hivi maisha ya ubinamu ndio yako hivi?

Denis:Kuna usemi unasema "Binamu nyama ya hamu". Labda binamu anataka kuprove kama ni kweli au ni usemi tu.

Clara :Ma Cousin ni  changamoto kweli kweli, mpotezee tu!

Benard: Mkuu, heshimu ndoa yako.. heshimu mke uliyemtukuza kuwa mama watoto wako.. "Utanusurika ukijinusuru!!"
Huyo binamu mnunulie zawadi akitakacho halafu mpe wife (mkeo) ampe kama zawadi... ila hizi tabia za baadhi za uswahilini huharibu nyumba nyingi na kusamabaratisha familya!!
usifunguwe mlango wa nuksi....



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni