Jumatatu, 1 Agosti 2016

CHUPI NA SHANGA ZALETA KIZAA ZAA!

Ni hivi mimi naishi nyumba ya kupanga na my wife wangu na kuna wapangaji wengine katika nyumba hiyo,kama unavyozielewa nyumba za uswahilini  sasa kuna binti single kahamia katika chumba kimoja katika hii nyumba,basi baada ya kuzoeana naye mke wangu anasema hamuamini ingawa nimemuhakikishia kuwa sijafanya naye mapenzi wala sifikirii,basi mke wangu akaanza kumletea vituko huyu binti mpaka wakagombana na hapa niandikapo ni kuwa hawaelewani.

Sasa tatizo leo hii yule binti kaingia maliwatoni na kuacha chupi yake akining'inia nyuma ya mlango,na shanga mbili!

Basi mke wangu naye akaenda kuniwekea maji maliwatoni ili nikakoge,basi nilipoingia nikaiona ile chupi nyuma ya mlango na zile shanga nikashtuka kidogo nikaanza kujimwagia maji baridi.

Lakini nikiwa naendelea kukoga ile chupi ikaanguka kwenye yale maji ambayo ni machafu,basi nikaona ngoja niisuuze ili niirudishe tena nyuma ya mlango na nimtaarifu mwenye chu pi kwa kilichotokea,basi nikiwa naisuuza ile chu pi mke wangu akaingia maliwatoni na kunikuta nikiisuuza ile chupi ya mpangaji mwenzetu,basi likaanza bonge la zogo na kuniambia kuwa kumbe yule mpangaji mwenzangu nina uhusiano naye yaani mpaka chupi namfulia na shanga ananioneshea!basi yeye kaamua kurudi kwao.

Yule mpangaji mwenzetu ikabidi nimuambie jinsi ilivyokuwa ili amuaminishe mke wangu kuwa hakunipa nimfulie ile chupi yake,lakini yule binti mpangaji mwenzetu kagoma kuongea na mke wangu kwa madai kuwa mke wangu anaringa sana.

Jamani nimechanganyikiwa sijazoea kulala peke yangu. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni