Jumanne, 2 Agosti 2016

DUME ZIMA HANDSOME HILIZI YA NINI

Ni Jumatano mchana, lunch time hours, nimekaa kwenye restaurant moja mjini nikila chakula, ghafla kaingia mkaka mtanashati sana, kapendeza haswa kifua cha haja na mabega yaliyokaa vyema ,ana jeans na viatu vya bei mbaya, ana bracelet ya dhahabu, cheni kubwa ya dhahabu na pete nzito. Alipoingia tu mgahawa mzima ukajaa harufu ya nzuri ya Sex Gravity for Men nzurii inanukia.
Akatembea taratibu na kuja kwenye meza niliyokuwa nimekaa, akaomba akae nami nami nikamkaribisha.
Nilipomaliza kula akaniomba ninywe japo glass ya wine ili tuweze kuongea kidogo na kufahamiana.
Mazungumzo yalinoga, tukabadilishana namba za simu na kuagana.
Ijumaa mchana tukakutana tena kwa ajili ya lunch, tukawa marafiki wazoefu, kucheka, kugonga na utani kiasi, tukakubaliana jumamosi tutoke usiku kwa ajili ya candle light dinner.
Dinner ilikuwa nzuri sana na ilisindikizwa na muziki mwororo, it was so good really, baada ya dinner tukaanza kupata ndovu (huwa sina muda wa ku fake na savanna au Heineken, mi yangu ni ndovu tu) Usiku mzito, akili zimeongezeka kutokana na wine ilishuka chini! tukaona ni muda muafaka kwenda kupumzika.
Katikati ya mchezo nikaanza kuhisi kuna kitu kinanikwaruzakwaruza, baada ya chezo kwisha tukalala kama wafu, nilipoamka nikakuta jamaa kalala ile mbaya, kiunoni ana hirizi halafu una bag kubwa kuliko kufuli la geti. Nilikasirikaje? Alipoamka nikamuuliza hii ni ya nini? Eti inamlinda yeye na mali zake. Nikamuuliza aliyekupa yeye ana mali nyingi kiasi gani?
Akasema hana mali, lakini anaiamini sana.

Kuanzia siku hiyo sitaki hata kumuona, asije akanitoa kafara mtoto wa watu kwa ajili ya uchu wake wa utajiri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni