Jumatatu, 1 Agosti 2016

TUNZA SIRI ZA MWENZANKO BASI

  1. Weekend hii bhana nilienda kumtembelea best angu mmoja hivi sasa katika tembeatembea tukakutana na mbaba mmoja hivi jirani ake, baada ya salamu akapita zake best akaniambia namuonea huruma kweli huyu baba siku atakapogundua tabia ya mkewe sijui itakuaje,

    Ni hivi huyu mke wa huyu jamaa ana tabia ya kusimulia madhaifu ya Mme wake kwa mashoga zake anadai kuna siku moja huyo mwanamke alikuwa anawasimulia;

    ''Yaani huyu mwanaume natamani nimuache hata leo kitandani hawezi chochote yani kinachonifanya niendelee kuishi naye ni kwa vile ananijali na ananipa kila nachotaka lakini kwenye swala la 6/6 ni sawa na ananichafua tu. Ila nina mtu ambae ananifikisha ninavyotaka''.

    Wakati anaawaambia hayo mara akapigiwa simu na mume wake basi akawaambia ''ngoja niende huyu ----- ananiita naona anaongea kwa ukali kweli sijui kapatwa na nini''.

    Anavyodai alivyofika kwake huko kamkuta mmewe kafura hatari kabla hajakaa kapokelewa na kibao hajakaa sawa kingine ''nini mume wangu mbona unanipiga nimefanya nini?''. Mume wake kwa hasira, ''nimekusikia yote uliyokuwa unawaambia mashoga zako''.

    Mwanamke akaachia kicheko akamwambia, ''Mume wangu hicho ndo kinakufanya unipige me pale nilikuwa najaribu kukulinda mme wangu kuna shoga angu mmoja nasikia anakutaka na anasema atafanya chochote il aweze kukupata, kwa hiyo nilifanya vile ili kumkatisha tamaa si unajua ninavokupenda Mme wangu''.

    Basi mwanaume akanywea akasema, ''basi samahani mke wang nilifikri una mtu mwingine zaidi angu'' mwanamke tena akamjibu ''ninavokupenda mme wangu njoo unipe haki Yang kwanza''.

    Basi walivyomaliza mchezo wao mwanaume akapitiwa usingizi, yule mwanamke kaenda kuwasimulia mashoga zake kila kilichoendelea alivyomaliza akawaambia ngoja nirudi asije akaamka akanikosa.

    Wakati anaudi kwake shoga ake mmoja akachukua simu akampigia simu akamwambia tunajua kila mlichokifanya mkeo kaja kutuambia mwanaume alichojibu huyu mwanamke vipi anatoka nje harakaharaka anakutana na kutana na mkewe mlangoni katoka kuoga kamuuliza unatoka wapi alichojibu ''mme Wangu si unaona nimetoka bafuni kuoga baada ya shuhuli pevu ulionipa?".

    Basi mwanaume hakuwa na la kufanya zaidi ya kufikiria kuna watu wanataka kuwachonganisha.

    Mimi kwa upande Wangu sikufurahishwa na tabia ya huyu mwanamke, hamtendei mwenzie haki hata kama ana mapungufu hakupaswa kumuacha mwenzie uchi hivi. Sijui ingekuwa ni wewe ungefanyaje?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni