Jumatatu, 1 Februari 2016

JINSI NILIVYOKWEPA CHANGA LA MACHO LA MIMBA YA MCHUMBA

Siku hizi limezuka wimbi kubwa la wanaume wengi kulea watoto ambao sio wao bila ya wao wenyewe kugundua yaani wanakuwa ni watoto wa goli la mkono , mara nyingi mwanamke humsingizia mtoto mwanaume yule mwenye malengo nae(kwa kiswahili cha mtaani tunaita  mwanaume wa display au wa shooting video ) au mwenye uwezo wa kulea mtoto yule, mara nyingi mimba za kwanza za ubinti huwa ni za kusingizia.
Nije kwenye yaliyonikuta mwenzenu miaka nane iliyopita nikiwa nimeajiriwa kwa mara ya kwanza kazi nzuri serikalini Agency mshahara mnono ata ata pombe sijaanza kuonja nilipata mpenzi mwanachuo akiwa chuo cha ualimu kabinti kazuri katamu yaani  nilikapenda sana huku nikijua ananipenda mara kwa mara alipokuwa anafunga alikuwa anakuja kwangu maana hata wazazi wake walijua uhusiano na mapenzi yaani ilikua mahaba niangamize!
Kuna kipindi alinilazimisha kuja kwamba huku akisisItiza kuwa amenimisi big time  nikamkatalia lakini akalazimisha kuja kumbe alikuwa tayari alikua na mambo yake ,akafika na kulala siku ya kwanza ya pili uku machale yakinicheza kwanini amelazimisha kuja kwa nguvu,kwaiyo mzigo sikula nikavunga kuwa naharisha tumbo .Mungu saidia siku ya tatu nae akaugua ghafla full kutapika halafu akawa analazimisha kuondoka nikamkomalia kumpeleke kwa nguvu hospitali nikamnong’oneza daktari aliyekua mshikaji wangu tulikua na mazoea ya kugonga “vyombo” bar moja jilani  kuwa  ampime vipimo lakini sanasana mkojo kucheki kwani nahisi ana “jipu” la mimba, majibu kutoka ana mimba kuumuliza akaanza kulia na kunieleza kuwa alichepuka na mwanachuo mwenzake mara akawa amebeba akaona anisingizie maana ananipendasana ,hahaaaaaaaa nilimtimua kama mbwa,ndio ikawa mwisho wa mimi na yeye.
Hivyo basi nawashauri wadogo zangu wa kiume kuwa ukiwa na mchumba ukaona analazimisha kuja kwako jiulize maswali mengi kwani wakati mwingine YES maana yake NO! ujue inawezekana kanasa huko anataka kukushikiza wewe kwasababu wewe ndo “husband material”cha muhimu akija mlie “taimingi” mpeleke hospitali au nunua kipimo na hakikisha mkojo anakojoa ukiwepo ili asikuwekee maji kwamba ni mkojo utapigwa mchanga wa macho Jombaa!

Kulea mtoto wa mwanaume mwingine inauma.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni