1. Japo maisha ni kusaidiana ni aibu na fedheha mwanaume
kulishwa na mkewe.
2. Ni aibu na fedheha mwanaume kuhamia kwenye nyumba ya mkeo
ukakala ukakoroma na taulo ukafunga.
3. Ni aibu na fedheha kuendesha gari la mkeo wakati wewe
hujawahi kumiliki gari alafu unawaka wivu juu yake.
4. Ni aibu na fedheha kuishi na mwanamke ambaye wakwe zako
wanajua kuwa anakuzidi uwezo.
5. Ni aibu na fedheha kumuoa mwanamke ambaye anamiliki
uchumi wa familia hata watoto anasomesha yeye wewe unajivunia uume mkubwa na
kwnenda chumvini sana.
6. Ni aibu na fedheha kila likizo unaenda kijijini kwa mkeo
na watoto wote kisa yeye anazohela.
7. Ni aibu na fedheha kukaa miaka mingi unamlaumu mkeo kuwa
hazai wakati wewe huna hata mtoto wa kusingiziwa.
8. Ni aibu na fedheha kumrudia mwanamke aliye kuacha yeye
mwenyewe kipindi kirefu na akaamua kukurudia yeye mwenyewe tena kwa masharti
kutoka kwake.
9. Ni aibu na fedheha kupewa zawadi ya kiwanja na wakwe zako
siku ya send off.
10. Ni aibu na fedheha kujenga kwenye kiwanja cha mkeo
wakati wewe hujawahi kumiliki kiwanja.
11. Ni aibu na fedheha kulelewa mtoto wako na baba wa kambo
wakati wewe upo unaishi na unajiita kidume.
12. Ni aibu na fedheha kukaa kwenye nyumba yenye fenicha
zoote kanunua mkeo.
13. Ni aibu na fedheha kusimamia ujenzi wa nyumba ya mkeo
wakati wewe huchangii hata shilingi mia.
14. Ni aibu na fedheha kulea mtoto ambaye sio wa kwako kwa
kisingizio cha kitanda hakizai haramu wakati mkeo anajua mtoto yule sio wa
kwako.
15. Ni aibu na fedheha kulala kimapenzi na mwanamke ambaye
anajua kuwa wewe unajua na unaushahidi wa michepuko yake.
16. Ni aibu na fedheha kumbembeleza mwanamke anayejua kuwa
anakukosea kwa makusudi.
17. Ni aibu na fedheha kumaliza makanisa ukiwahadithia
wachungaji tabia mbaya na usaliti wa mkeo.
18. Ni aibu na fedheha mkeo kukunyima unyumba ukaenda
kumshitaki kwa wazazi wake wakati unajua cha kufanya.
19. Ni aibu na fedheha v mara kukopakopa kwa wakwe zako tena
waliostaafu kazi..ni aibu ni aibu kubwa.;
20. Ni aibuu na fedheha kwenda baa na mke baa au sehemu za
starehe kila siku ikija bili unapewa wewe nawe unampa mkeo alipe kazi kukuna tu
kidevu na kwenye wallet umejaza business card na viwembe vya kugushi nyaraka
mitaani.
Hizo ni baadhi tu ya aibu za wanaume waliowengi karne ya
leo. Sambasa wajijue na wamuombe Mungu awafungulie milango nao wawe wanaume
katika nyumba zao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni