Jumatatu, 1 Februari 2016

WADADA MUJIFUNZE KUWA NA SIRI BASI!

Najua wanawake siku hizi wana uhuru kuliko zamani lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa hata zamani wadada walikuwa wanajipa good timevilevile kama sasa ingawa teknolojia zinatofautiana.

Tatizo lenu wadada sikuhizi hamna siri!

We angalia kila kitu kuhadithia mashosti. Kila utakayetoka naye unaonyesha watu. Kila utakachopewa kila utakapopelekwa (i.e hotels,beach,outdoors) tutaona picha istagram,face book ,wengine ujisahau na kuanza kusifia mpaka gemu alilolopewa na fulani lol! bidada mmemzidi!
Sio tu utasababisha sasa kama ni bwanako akija kama ni kazini au hostel watu waanze kumwinda sasa!hahahaaaa pole utalia na wenzako watakula samba na wewe kimya kimya tena bila wivu!si umewaoneshea “windo” la Nyati aliyenona!
Kwani umezaliwa nao tumbo moja?. Ukipewa hela kila wakati wewe kutulushia mapicha sijui mara Splash Mlimani City ,mara Wool Worth Posta, mara Nairobi  five star kwani nasisi hatutamani kwenda uko?shauliyako bwanako huyohuyo nae tutaenda lalanae uko!
Wengine mnapelekwa guest tu lakini tutaona picha ya dinner na breakfast za kizaramo. Mbona wenzenu wanapelekwa 4 stars wamekausha!
JIFUNZENI USIRI.
Acha love,sex life yako iwe private. Ukiji praudi sana na kutooneshea mmeo akija tu lazima tujibinue makaliona kufungua vifungo viwili vya baluzi kifuani ooh! joto!habari ndo iyo!mumeo mume wetu sote!hahaahahaaa!
 Usihadithie mashosti,kwani kila shosti unaemuhadithia lazima atatamani nae kimya kimya !yaani moyoni ataumia wewe hutajua ila kosa moja magori mia!akikutana nae bwanako Mlimani City imekula kwako kwani ni full kujirahisisha tena siku hiyohiyo ataanza shemeji nina kiu ya bia nipeleke Calabash napenda sana live bendi!Wakifika uko shostito atajimwaga full kuachia mapaja wazi kwa shemeji ili bia ikikolea shemeji ajiongeze mwenyewe ikigoma hiyo utasikia nawewe unajifanya umepata mwanamke wakati  hana lolote si ni m#laya mwenzetu tu yule!Habari zake zote ninazoe niulize mie tena ukimshusha saloon huwa tunakuonea huruma!.
 Ukipitia,ukalala hotelini wakati unajua unaishi kwenu au hostel, au unajua unataka kuonekana mtu wa dini, achana na hiyo camera.
Usije shangaa kesho unaachika fasta baada ya mashosti kumjaza chifu maneno kuwa mwezi uliopita  mimba uliyotoa haikua yake bali ya mwalimu wa chuo alikunyofoa sup  au  dereva wa bodaboda wako!
Hupungukiwi kitu. Zoea kusema sina mtu sanasan nyie  wadada wa chuo mlio na pressure za kushow off mabwana. Itawasaidiasana.
**you wanna be "that" good lady at 30? Don't get caught at 20.
Afu wanawake tunajuaga kurushana roho jamani. Kuna mtu anaweza akakusimulia mambo yake kwa mfano, boyfriend wake anavyo mtreat kumbe muongo mkubwa.
Hii ilishawahi kutokea kwenye  bufee ya kampuni moja kubwa hapa Dar es Salaam wakati wa mlo binti alianza kuwarusha roho wenzake yupo kwenye foleni ya chaklula kuwa oooh baby niletee take away huku bufee la leo halihamasishi pitia Steers niletee beef berge mbili ……
Sasa kwakua mimi niliohisi anadanganya na namba yake ya simu nilikua ninayo nikamtwangia simu hapohapo kwneye foleni kwanini simu isilie sikioni kwake uku anaongea!watu wote walishikwa na butwaa na kuanza kucheka !

“Mmmmh Jack muda wote unaongea na dear kumbe uongo!”
 Ndo wale wanaojinunulia hadi zawadi afu anadanganya wenzie kanunuliwa na baby. Aonekane tu yeye ndo anapendwa sana, yeye ndo anaenjoy mapenzi sana mmh, akili kumkichwa. Unaanzaje kusimulia ulivyolala na mtu mmh? What for?
Uzuri wa haya maisha kila generation huona wazazi wao ni washamba na kwahiyo kamwe ma teenager wamiaka 20 ijayo hawatafanya upuuzi wowote tunaushuhudia hivi sasa God forbid
Nope kuna kukua kimwili, kiroho na kiakili ujue. So watakua tu kiakili siku moja


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni