Jumatano, 10 Februari 2016

UKIENDA NA MKE WAKO UKWENI(KWAO) USILALE NAE MBALI

Mahali ninaposhi kuna nyumba zipo kama tatu hivi ndani ya ua mmoja ,sasa jana jioni nilivyorudi kutoka kazini niliitwa na mke wa jirani kujaribu kusuruhisha ugomvi  kati ya mume na mke ingawa baada ya wao kutoka rikizo ,hatukufanikiwa kwani mwanaume aligeuka mbogo na pasipohitaji suluhu yoyote na mkewe,
Kisa kilikua hivi ,wakati wakiwa wanatoka likizo kwa wazazi wa mwanaume waliamua kupitia kwa wazazi wa mwanamke japo kukaa hata siku mbili yaani ukweni kusalimia, sasa zogozogo lilianza hapa, baada ya kufika kwao mwanamke, walikaribishwa vizuri na wakaoga, wakala na sasa ikafika zamu ya kwenda kupumzika. Sasa mwanamke kumbe alikuwa ameshamtaarifu boyfriend wake wa siku nyingi hapo mtaani kwao kwamba nitakuja siku fulani, siku hiyo wakati wa kulala, mwanamke alikataa kulala na mumewe ndani ya nyumba yao ( (nyumba ya ba mkwe), eti akidai (mwanamke) kwamba siyo vizuri kulala pamoja eti yeye na mumewe kitanda kimoja kwenye nyumba ya baba yake, akihoji je, ikitokea "mwanaume akahitaji mchezo itakuaje?Kwani mwanamke huwa anapiga sana kelele wakati wa tendo na wazazi watasikia”!
Basi jamaa (mumewe) ikabidi awe mpolekwa shingo upande  akamruhusu mkewe akalale chumba kingine lakini ndani ya nyumba hiyo, sasa mkewe akatumia mwanya huo, kufungua mlango na kwenda kwa ex boyfriend wake wa muda mrefu, anaekaa nyumba ya tano kutoka kwao kwa bahati mbaya mambo yalinoga sana usiku akajisahau mpaka saaa kumi na moja alfajiri akarudi .
Wakati anarudi akakutana na baba yake nje ( ambaye ni ustaadhi  akijiandaa kwenda  swala) nje, ndo baba yake akaanza kumuuliza anatoka wapi usiku huo na yupo peke yake, mumewe yupo wapi! Kumbe wakati anamuhoji mkewe, mume  alikuwa macho akupata usingizi alisikia kila kitu maana dirisha la chumba alicholala mumewe lipo upande wa getini, mke wake alishindwa kutoa jibu lolote  huku akiomba radhi kwa baba yake tena kwa sauti ya kunong'oneza sana.

Kulipopambazuka mume aliamua kupiga kimya akapotezea na alikaribishwa chai akanywa na baadae akaomba kuondoka ili kuwahi kazi akidai likizo yake ilikuwa imekwisha.Wakaondoka pamoja na mkewe, sasa kufika nyumbani ndo maswali yakaanza.
Ndio zogo kubwa likafumuka kwa jirani , na ikabidi mwanaume ampe nauli mkewe arudi kwao kwanza ili atafakari hatua nzuri za kuchukua dhidi yake.

Kiufupi, Mwanamke alikomaa bila ya kukubali kosa, alikataa ila mmewe alipomuuliza swali aliloulizwa na baba yake juzi na jibu ambalo yeye alimjibu baba yake ndipo mwanamke akaishiwa nguvu,na kuanza kuangua kilio kikbwa tukadhani kuna msiba!Mumewe alimwambia nguo aliyovaa siku hiyo ya alfajiri na baba yake alivyokuwa amevaa siku hiyo ya alfajiri.

Sasa ndugu zangu wanaume kazi kwetu kwa wale mliooa tayari kazi kwenu, sisi wengine tunajifunza kwanza. Jana baada ya kutoka kazini, nilikuta ugomvi kwa jirani yangu ambaye alikuwa ameenda likizo na mkewe sasa wakati wanataka kurudi kazini ikabidi wapiti kwao mwanamke kuwasalimia, sasa zogozogo lilianza hapa, baada ya kufika kwao mwanamke, walikaribishwa vizuri na wakaoga, wakala na sasa ikafika zamu ya kwenda kupumzika.

Sasa mwanamke kumbe alikuwa ameshamtaarifu boyfriend wake wa siku nyingi hapo mtaani kwao kwamba nitakuja siku fulani, siku hiyo wakati wa kulala, mwanamke alikataa kulala na mumewe ndani ya nyumba yao binti (nyumba ya ba mkwe), eti akidai (mwanamke) kwamba siyo vizuri kulala pamoja eti yeye na mumewe kitanda kimoja kwenye nyumba ya baba yake, akihoji je, ikitokea "mwanaume akahitaji mchezo"?

Basi jamaa (mumewe) ikabidi awe mpole amruhusu mkewe akalale chumba kingine lakini ndani ya nyumba hiyo, sasa mkewe akatumia mwanya huo, kufungua mlango na kwenda kwa ex boyfriend wake wa muda mrefu, akarudi asubuhi ya saa 11 alfajiri.

Wakati anarudi akakutana na baba yake nje, ndo baba yake akaanza kumuuliza anatoka wapi usiku huo yeye peke yake huku akihoji mume wake alipo! Kumbe wakati anamuhoji mkewe, mumewe alikuwa anasikia maana dirisha la chumba alicholala mumewe lipo upande wa getini, mke wake alishindwa kutoa majibu yoyote huku akiomba radhi kwa baba yake tena kwa sauti ya kunong'oneza sana.

Kumbe mumewe alisikia yote na alipoamka alikaribishwa chai akanywa na baadae akaomba kuondoka ili kuwahi kazi akidai likizo yake ilikuwa imekwisha.Wakaondoka pamoja na mkewe, sasa kufika nyumbani ndo maswali yakaanza na ugomvi mkubwa umetokea jana, na ikabidi mwanaume ampe nauli mkewe arudi kwao kwanza ili atafakari hatua nzuri za kuchukua dhidi yake.

Kiufupi, Mwanamke hakukubali kosa, alikataa ila mmewe alipomuuliza swali aliloulizwa na baba yake juzi na jibu ambalo yeye alimjibu baba yake ndipo mwanamke akaishiwa nguvu, mumewe akamwambia nguo aliyovaa siku hiyo ya alfajiri na baba yake alivyokuwa amevaa siku hiyo ya alfajiri.


Sasa ndugu zangu wanaume kazi kwetu kwa wale mliooa tayari kazi kwenu, sisi wengine tunajifunza kwanza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni