Jumatano, 10 Februari 2016

NIMETUMA MESEJI HII KIMAKOSA KWA MAMA MKWE!

Habari zenu wapendwa,

Natumaini  mpo salama japo kwa upande wangu sipo salama sana nimechanganyikwa leo mbayaaaa!mpaka ninavyoandika uzi huu nimeshindwa hata kwenda kazini na hapa moyo wangu unaenda mbionaombeni msaada kwenu  wa kiushauri na wa kimawazo naweza hata mkanipoteza katika dunia hii kwa presha niliyokua nayo hapa nilipo ,nimeshindwa hata kuwasha gari !akili zangu nahisi hazipo timamu kwa sasa!
Ukweli ni kwamba nilikuwa naandika SMS kwa mchepuko wangu uitwao Roswita au (mama Jane) na kwa bahati mbaya sana wakati natuma nikakosea namba na kutuma katika namba ya mama mkwe wangu na meseji ikawa sent and delivered.Kwenye simu yangu nimesevu jina lala Mama Jane sasa kwa kuwa jina lipo karibu na jina la “mama mkwe” nikajisahau na kubonyeza sent alafu OK kwa bahati mbaya!Nikajikuta tayari meseji ipo kwenye sent item na mara baada tu ya kituma ghafla mama mkwe akanipigia zidi ya missed call ishirini hivi  ila kwa kuogopa na aibu nimeona nisipokee na nimezima simu kabisa.

Na kwa dalili ninazoziona ni lazima tu atakuwa ameshamtaarifu na pengine hata kum-foward ile SMS mke wangu Magie maana nampigia simu hapokei ila amenitumia meseji inasema “sasa ndo umefanya nini mume wangu!” sasa sijui leo kama patakucha akiludi baadae  maana ndo ameshakwenda kuwajibika tayari kazini.

Meseji yenyewe niliyoituma ni hii " Mambo vipi Roswita Bonita ! Hujambo? Umeamka salama? Vipi si tayari umeshamaliza period yako na leo naweza kuja ukanipa mambo love?unipe na ile tamu tamu honie!Zingine nizibakize kwa dada yako “baby wife” wangu maalum kwa siku ya Valentina  Jumapili hii kwani ni haki yake ya kindoa. Utaninunulia Wine gani leo ili nikuchangamshe vizuri kama unavyopenda?Honie usisahau na yale mafuta basi!Baby uvae ile bikini ya purple na mechisha na ile bra yake! Halafu ulisema unataka hela sijui ya kununua nguo ila kwakuwa ili li mke langu nalo eti linataka hela sasa ngoja kwanza nilidanganye kuwa sina na lisubiri hadi nipate ila wewe mke mdogo  nakutumia sasa hivi sawa? Si ulitaka Tsh laki 1? Sasa nakutumia Tsh Laki 2 na nusu hizo zingine utajua utanunua nini au utaitumiaje sawa baby?
 Nijibu na tambua sitokuacha kamwe mwaaaaaah Loswita ".


Hiyo ndo meseji niliyotuma najua kimeshanuka sijui nikimbilie wapi?Nilipiga simu kwa jamaa yangu yupo Telecom company ikiwezekana aisimamishe iyo meseji hewani nimpe hata laki tano imeshindikana kabisa!mnijibu haraka basi ili niweze jipanga kuzipangua hoja kama hali ikiwa mbaya kweli.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni