Jumatatu, 1 Februari 2016

AINA KUMI ZA NDOA HIZI HAPA.

Leo hii tutaona aina kumi za ndoa kama ifuatavyo:

1. NDOA YA MKEKA
Inatokana na kufumaniwa na Binti wa watu.Ndoa hii huwa Haina mahari. Hii huvunjika mwaka mmoja tu,baada ya wanandoa kugundua hawakuwa wakipendana!Ni maarufu sana kwenye miji ya Pwani san asana uswahilini.

2. NDOA YA MIHEMKO (NYEGE)
Hufungwa na vijana wa kiume  wenye umri wa miaka kati mume 22 mpaka 25  na  mke miaka 19 mpaka 23.Mara nyingi vikao vya harusi uanza pindi kijana anapokuwa amepata kazi baada ya kumaliza elimu ya chuo na uvunjika baada ya miaka 2 au 3 ya ndoa,kwani wanandoa wanakua sio wakomavu(mambo mengi ya mihemko kama vile kuchepuka nje ya ndooa wanakuwa hawana uzowefu nayo).

4. NDOA YA MAONYESHO
Wenye ndoa hii hupenda kujionyesha barabarani na mara nyngi wanandoa hasahasa wanawake ufose kingi aolewe kwa ajili ya mashindano tu na shoga yake kwasababu nao wameolewa basi nayeyey lazima aolewe tu ili kuondoa mkosi tu,na mara nyingi ndoa inakuwa ni ya ukumbini tu lakini rohoni hamna kitu.Ila ndani hazina utii.Hupigana kila wanaporudi kutoka kwenye mizunguko. Cha kushangaza huwa hazivunjiki lakini ndiyo ndoa zinazoongoza kwa kuchepuka!

5. NDOA YA UHAMISHO.
Hufungwa na watumishi wa vijijini na mjini. Ili wa kijijini ahamie mjini.Mahari utoa anaetaka kuhamia mjini. Hata kama mahari atatoa mume lakini hii ndiyo ndoa yenye ukakasi zaidi.Huvunjika mara tu wanapoanza kuishi wote mjini. Salama ya hii ndoa ni kuhama kutoka mjini kwenda kijijini.

6. NDOA YA MIMBA.
Hufungwa kwa sababu wanaoowana hawataki kuonekana makwao kuwa wamezaa nje. Au muolewaji alikuwa hampendi muoaji kwa dhati.Mara nyingi muolewaji hutumia mimba kama mtego wa kuingia ndoani. Hii huvunjika mtoto akizaliwa na kufikisha mwaka 1 au 2.Mara nyingi utengenezwa na mabinti wa mjini hasahasa wasomi   au wenye kipato na kazi nzuri.Hapa mara nyingi muolewaji anakua ameshapata kila kitu katika maisha kasoro mume tu!

7. NDOA YA MALI (UTAJIRI)
Muolewaji miaka 18 au 28 Muoaji 65 au 70.Ndoa hii pia huitwa ndoa ya babu na mjuukuu. Ndoa ya aina hii hudumu, kwasababu mwenye kauli ni mwenye mali. Asilimia kubwa ya waume wa ndoa hizi hulea watoto wasio wao.

8. NDOA YA KWASABABU.
Hufungwa ili mradi muoaji au muolewaji aonekane tu kwa jamii kuwa naye kaoa au kaolewa.Huwa hazina utii wala upendo dhati. Ndoa ya aina hii ikifikisha miaka 4 huwa hazivunjiki wahusika huishi kwa ajili ya mazoea na watoto.

9. NDOA YA UPENDO.
Ndoa hizi ziliishia mwaka 1978 kabla ya vita vya kagera.Muoaji na muolewaji hawakuangalia vitu ila utu tu ambao uliwaunganisha na kutengeneza upendo wa kudumu. Hii ilidumu miaka yote.

10. NDOA KUCHUMA

Ndoa hii ufungwa ili mradi muoaji au muolewaji akapate kitu au vitu Fulani(kama vile kazi,mali,umarufu,tenda) kutoka kwa mpenzi wake au wakwe upande upande wa pili . Hii hudumu miaka kadhaa kutegemea na malengo ya mhusika. Wengine husubiri mpaka mhusika afe,lakini hujikuta wanakufa wao kwanza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni