Jumatatu, 1 Februari 2016

WIFE KAKUTANA NA EX WAKE KAFURAHI HAKUNA MFANO!

Wadau mambo vipi?
Kuna jambo limeikoroga akili yangu sana juzi naomba niwashirikishe kidogo. Jumamosi iliyopita mimi na wife tulienda kula bata maeneo ya Villa Park hapa  Mwanza nyakati za jioni baada ya kutoka kufanya shopping hapo Rock City Mall maeneo ya Ghana. Wakati tumefika maEneo ya Nyegezi tukielekea mjini wife alinambia nisimame kidogo kuna rafiki yake yupo saloon ambaye nilikua namfahamu tangu wakiwa chuo Saut  Nyegezi , nae alikua anaelekea hukohuko Rock cCity Mall tumchukue, akampigia girlfriend simu aje barabarani . Hivyo tukawa watatu kwenyegari mpaka  mizunguko ya huko mall; mimi, wife na girlfriend ambae alikua family friend kwetu ingawa mimi sina mazoea nae kiiivile.
Kwa kuwa ilikua mida ya saa kumi na moja jua lilipoanza kuzama tukaamua kukaa Villa Park kwa ajili ya kusubiri kusakata rhumba na kwa kuwa wwife huyu alikua ni shaga yake hasa sikua na option zaidi ya kuwaacha wahe huru uku mimi nikiendelea kugonga Konyagi yangu kubwa na better lemon  na wao walikua wanakunywa Saint Anna moja wawili, tukakaa karibia na kaunta ya chini  nje. Kwenye saa mbili kasoro usiku akajitokeza jamaa mmoja kwa sura simjuhi kabisa ,baada ya kutuona akaja kutusalimia, ambapo wife aliinuka kwa shangwe kubwa na kumlaki kwa hugs na zile kiss za mashavuni wanazopiganaga wale wanaojifanya wazungu,jamaa likamkumbatia wife kwa nguvu.Nilipata kawivu kidogo lakini nikajikaza kiume!
Wife akanitambulisha kuwa "he is a longtime friend,huku nikiendelea kumtazama kwa mashaka kwani nilihisi zile mbwe mbwe zote za kukumbatiana pale kuwa sio ‘genuine’ lazima kuna kitu au kulikua na kitu fulani zamani,haiwezekani,hamna hapana!kuna kitu tu!". Jamaa akaita weita na akazungusha mbili za vinywaji, alafu akaniomba aende akamtambulishe wife kwenye meza yao kwa rafiki zake ,sikupendelea hiyo hali lakini kwa kuwa nilimuona wife ana muhemko fulani wa bashasha ya kukutana naa “friend wa zamani” nikakubalitu kwa shingo upande  ingawa moyoni nilikua nimefura kwa hasira, sema sikutaka kuonesha, bahati mbaya zaidi meza ya hiyo aliyokua ametokea huyo jamaa  ilijaa wanaume pekee.
Tukabaki wawili wakati wife anaongea na meza ile, yule girlfriend akasema "shemeji naomba namba yako hapa mjini huwezi kujua ya kesho na keshokutwa", nami nikajibu ni kweli kabisa, tukabadilishana namba.Monday yule binti akanipigia simu nikiwa kazini akaniambia shemeji kuna jambo nataka kukuambia ila usinitaje, nikajibu poa, akasema, "Yule jamaa wa jana ni ex wa mkeo. Walikua wapenzi kwa miaka yote mitatu chuoni wakiishi chumba kimoja nje ya chuo kama mke na Mume".
Na kwamba kwa kipindi chote cha hiyo 3 yrs alitoa kama mimba 2 hivi za huyo mshikaji, pia uhusiano wao ulienda hadi mtaani after university life. Walikuja kuachana kila mtu alipopata kazi yule ndugu akapelekwa Songea. Since then hawajawahi kuonana hadi hiyo jumapili pale Lock City Mall,Mwanza na kwamba ile njemba limerudishwa hapa Mwanza na halijaoa bado ila lina mapene sana.
Binti huyu alinibembeleza sana kuwa nisimtaje kabisa kama yeye ndie source ya hiyo habari. Huyu binti ni rafiki wa wife tangu chuo ila bahati mbaya ndoa yake ilipata shida kidogo na kushindikana kutokana na uzinzi wa mwanaume.Niliporudi home jioni ya monday nikaamua kulianzisha, ambapo wife alidai hakuona busara kunitambulisha kwamba yule bwana alikua ex wake.
Nikamuuliza ilikuaje ukafurahi na kushangilia kiasi kile na kushindwa kuficha kabisa hisia zako? Akabaki anajiuma uma tu na kushindwa kujibu.
Kiukweli sijaridhika na majibu yale na bado nafanya uchunguzi.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni