Ijumaa, 15 Januari 2016

AKA KATABIA KANAKERA MNOOO!

Nimeingia Club nakuona kwa mbali,Demu mzuri umetupia vitu hatari unawakawaka na kunyemka vizuri kwenye dancing floor,Watu wote wanakutumbulia macho huku ukiendelea ku dance kwa haiba ya aina yake.
Naendelea kuangaza macho kulia na kushoto nakaza moyo nakupotezea na kuamua kupanda ngazi kuelekea kaunta ya juu.Baadae tunakutana tena umekaa kaunta ya chini unakunywa Ndovu Lager,Tunasalimiana naomba kukaa karibu nawe unanikubalia,namwita weita hakusikilize unaamua kuagiza Dompo!Najisemea moyoni aiseee hii atalipa mwenyewe tuu,kwasababu hamna namna nyingine yeyote!Nilishamwambia weita kuwa nitalipa Ndovu lager pekeyake.
Vinywaji vinakuja namlipa weita arafu nakuomba excuse kuwa gari limepaki vibaya nje lakini ndo nasepa sasa!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni