Jumatano, 13 Januari 2016

YALIYONIKUTA BIBO HOSTELI

Ilikua siku ya Ijumaa nikiwa maeneo ya Buguruni  kwenye bar fulani karibu na kituo cha polisi baada ya kupokea "boom" la bodi ya mikopo nikiwa chuo kikuu Dar es Salaam kama mwanafunzi wa degree ya sheria maisha ya hosteli hayakuwa magumu na nilikua naishi Hosteli za Mabibo zikijulikana kama Bibo Hostel.Baada ya kuanza kuonja bia tatu hivi nilizidi kuchangamka na kuanza kuchangia stori za mambo ya uchaguzi na mdada mrembo aliyekaa meza ya jirani nami nae nilimrushia bia mbili za haraka haraka huku nikimuonesha ishala kama anaweza jumuika kwenye meza yangu.
Baada ya nusu saa mdada alijumuika kwenye meza tukaendelea kuongea kuhusu uchaguzi mkuu na jotolake,ndipo tukaanza kufahamiana kwa undani na yeye alijitambulisha kama mwandishi wa habari wa chombo kimoja maarufu  nchini na mimi nikaona haitakua vyema kujitambulisha kama mwanafunzi wa Udsm kwani ataniona sina hela niliamua kujitambulisha kama "Ofisa Usalama wa Taifa".Kadli bia zilivyozidi kumiminika mezani kutokana na maelekezo niliyowapa wahudumu ndivyo uzuri wa binti ulivyozidi kuongezeka na kuwa mrembo sana tuliendelea na mazungumzo uku mara mojamoja tukiinuka na kusakata rhumba  mpaka tukafikia muafaka wa kwenda kulala pamoja huku tukiitana baby.
Siwezi kumbuka kilitokea kitu gani lakini  asubuhi ya siku iliyofuata niliamka nikiwa na shati,suruwali tu sina saa,walet iliyokuwa na Tsh 350,000.00 taslim,I-pad wala viatu.
Niliamka kama  saa tano asubuhi uku nikisikia maumivu makali kichwani nahisi aliniwekea madawa ya kulevya kwenye chuchu zake zilizokua zimeiva kama embe dodo mtini.Niliwaomba uongozi wa lodge waniazime kandambili nivae ili nirudi Hosteli kwani nilikua sina viatu wala pesa ya kuwalipa kwa ajili ya kulala. Nilijikonoja kwa miguu kutoka Buguruni mpaka Tabata relini kwani nilikua sina ata nauli ya Daladala!Nilipofika hostel niliwadithia wanafunzi wenzangu mkasa ulionikuta wakanichangia harambee ya sh 5,000.00 kila mmoja na walikua kama 50  nilipata kama tsh 250,000.00.
Siku azigandi ilipita siku wiki atimae mwezi huku sura ya yule dada niliyelala nae siku ile kule Buguruni haikuweza nipotea kichwani.
Kuna siku moja nilikua napita kwenye sehemu ya Miadhala ya Kijamii nikamuona mtu kama yeye akiwasilisha pepa mbele nikasimama na kuanza kumwangalia  mmmmh! nikaona mbona anafanana na yule binti niliyelala nae kule Buguruni!Nikavuta subira kwanza ili amalize muadhala.
Baada ya muda wanafunzi wakaanza kutoka kwenye Hall nikabana mlangoni nikiangalia mtu mmoja hadi mwingine mlangoni!Mara ghafla uyoapo mlangoni nikamvuta mkono na kumuuliza unanikumbuka?
Akajibu hapana sikukumbuki na sikujui nipo bize sasa!
Nikamvuta mkono tena na kumkata mtama mlangoni!wanafunzi wakataharuki!
Nikamuuliza tena unanikumbuka?
Akajibu nakukumbuka kausha bwana!
Nikamjibu kama unataka niokaushe lete walet yangu pamoja na hela Tsh 350,000.00 viatu I-pad na simu zangu mbili!
Wakati hayo yote yanafanyika baadhi ya wanafunzi waliwatonya askari wa pale chuoni kuwa kuna ugomvi kwaiyo ndani ya robo saa tukawa tumeshazingirwa na polisi wa chuoni!
Baada ya kujieleza tulienda mguu kwa mguu mpaka kwenye chumba alichokua amepanga yule dada mrembo maeneo ya Msewe na kukuta kwenye sanduku lake ana line za simu kama mia moja hivi.Niliweza fanikliwa kupata simu yangu ,i pad,pamoja na hela zangu taslim tsh 350,000.00
Ama kweli kutojua jambo ni sawa na usiku wa giza!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni