Jumanne, 5 Januari 2016

MSHENGA AMFUMANIA BIBI HARUSI!

Poleni na kazi najua wengi macho na masikio yenu yapo kwenye mifuko mkitafakari namna mlivyotumia pesa vibaya wakati wa msimu huu wa sikukuu za Chrissmass na mwaka mpya.Jana mida ya saa moja jioni nikiwa na ka mchepuko kangu tunaingia Sisimka Gesti House ili kujipumzisha na kupunguza stress za maisha baada ya kulipia chumba na kumwacha "mgeni" wangu chumbani nikatoka nje ili kuagiza mhudumu vinywaji atuletee.
Nikiwa koridoni nakutana uso kwa uso na mke wa rafiki yangu akitoka kwenye chumba kimojawapo na jamaa flani sura ngeni simjui anaonekana sio mweneji wa maeneo haya ile kuniona tu shem akastuka sana!
Jamaa alimuuliza kaulikoni jakujibu kitu zaidi ya kuondoks kuelekea nje,mi nikarudi chumbani na kuendelea na mambo yangu.
Usiku mida ya saa tatu kanitumia sms hii  "shem nakuomba sana usimwambia mtu ulichokiona leo!"
"Please naomba fanya tuonane kuna kitu nataka kukuambia naomba kesho ukiwa free nambie,nikukute wapi,nisaidie kwa hilo shem nami nitajitahidi kwa lolote".
Sikumjibu kutu leo asubuhi tena kanitumia meseji,"hi!shem huwezi amini usiku kucha sikulala nawaza mme wangu akijua nimekwisha!"
"Najua upo bize kazini nambie saa ngapi nikutafute tuongee wawili kiutu uzima jamani!"
Nikamjibu asijali siwezi kumwambia rafiki yangu vinginevyo ningeshampigia tangu hiyo jana.
Sasa shem ameendelea kukomaa anataka tuonane eti tuongee kikubwa!
Ni mzuri kaumbika mpaka mi mwenyewe udenda uwa unanitoka nikimuona sema tu mke wa mtu ni sumu!Alafu mme wake ni rafiki yangu tangu shule na ni mimi niliyekua mshenga wake!Naogopa kumwambia mshikaji kwani nahofia kuvunja ndoa yao ambayoa hata mwaka haijamaliza.Kinachoniuma zaidi ni kuwa mmewe ni Gentleman namjua fika hanaga tabia ya kuchepuka tangu zamani!
Najua lengo la huyu shem anataka kuonana na mimi ni nini.Mpaka sasa mdada anapiga simu eti nimjibu tukutane wapi na saa ngapi.
Sijamjibu bado natafakari nichukue uamuzi gani.

Maoni 1 :

  1. Huu ni lazima ushuhudia usomaji na kila mtu, nipo hapa kuruhusu ulimwengu wote kujua kuhusu mtu aliyeokoa uhusiano wangu na mtu huyu mkuu anaitwa Dr IZOYA. Hakika alifanya kazi nzuri kwangu kwa kumrudisha mpenzi wangu wa zamani ambaye aliniacha na kuahidi kamwe kurudi kwangu tena. Kwa hili, nimekuja kutambua kuwa kutoa maelezo ya Dk IZOYA kwa ulimwengu utafanya mengi mazuri kwa wale walio na nyumba zilizovunja au uhusiano kwa ajili yake ili kukusaidia kurekebisha uhusiano huo uliovunjika au ndoa yako. Unaweza kumfikia kupitia anwani yake ya barua pepe: drizayaomosolution@gmail.com au kumwita moja kwa moja kwenye [+12098373537]. Kuwasiliana naye na kuona jinsi tatizo lako litatatuliwa ndani ya 24hours. Pia mtaalamu katika mambo yafuatayo ...
    (1) Unataka kurudi nyuma yako.
    (2) Unataka kukuzwa katika ofisi yako.
    (3) Unataka wanaume / wanawake kukufuate.
    (4) Unataka mtoto.
    (5) Wewe ni mjasiriamali na unataka kushinda mikataba
    (6) Unataka mume wako awe wako milele
    (7) Unahitaji msaada wa kiroho.
    (8) Umeshambuliwa na unataka kupona fedha zilizopotea.
    (9) Weka talaka
    (10) Kualika kwa mila ya fedha
    (11) Chagua uchaguzi

    JibuFuta