Jumatano, 13 Januari 2016

AMTWANGA TALAKA MKEWE BAADA YA KUGUNDUA KUWA ALIKUA ANAZICHAPA NGUMI KUGOMBANIA BWANA STENDI!

Songombingo na vuta nikuvute lilitokea huko Arusha maeneo ya Kijenge Juu baada ya bwana mmoja(jina tumelihifadhi)kumtwanga talaka mkewe punde baada ya kugundua kuwa wife alizichapa kavukavu na kabinti kwenye standi ya basi kisa ni kugombania bwana!Sakata ilo la video ya bure ya kuchaniana skirt mpaka blauzi lilitokea katikati ya Stendi ya mabasi mchana kweupe ilifanya wapiga debe wazidi kushangilia na kupiga miluzi badala ya kuamulizia huo ugomvi.
Kwa mujibu wa mpasha habari hizi inasemekana kwamba hiyo siku mamsapu huyo wa "muheshimiwa fulani"aliaga kuwa anasafiri kwenda kwao Tengeru kwa ajili ya kicheni party ya shoga yake mtaani kwao.
Na siku ya tukio ndio ilikua siku ya miadi kati ya mke wa mtu na serengeti boy anaejulikana kwa jina la Dani ambaye kazi yake ya kujipatia ujilia wa kila siku ilikua ni kupaka rangi kucha akina mama.Muda ulipotimia inasemekana simu ya Dani ilikua haipatikani hivyo kusababisha mke wa "muheshimiwa" kupandwa na ghazabu ya hali ya juu.Baada ya muda mamsapu aliwasha Alteza na kuanza kupiga "doria bubu" sehemu zote alizohisi Dani anaweza kuwepo pasipo mafanikio.
Baadae mamsapu aliamua kusimama karibu na stendi ya mabasi ili anunue vocha ndipo video ilipoanzia hapo,kwani alimkuta Dani ndo kwanza anapanda ki Ford akiwa ameambatana na binti mwenye shepu nzuri makalio makubwa makubwa kuliko ya "mke muheshimiwa".Hapo ndipo presha ilipompanda "mama muheshimiwa" na kuwasha gari na kuanza kuifukuzia Kiford na ku block kwa mbele mithili ya ana ugomvi na dereva wa hicho ki Ford.
Alishuka kwenye gari uku dereva wa ki ford akishikwa na bumbuwazi Jjuu ya kosa gani alilofanya ndipo mke wa mtu alienda mpaka dirishani akimwamuru Dani ashuke kwenye basi na uyo "malaya" wake!
Mdada aliyekuwa na Dani hasila za mkizi zilimpanda na kumjibu kuwa "mimi si malaya!malaya ni wewe umeacha mmeo kazini,unachepuka tu!huna shukurani kwa mmeo subiani mkubwa!"Watu wote waliokua kwenye basi wakaangua kicheko na mke wa mtu akamzaba kibao mdada ndipo timbwili timbwili lilipoanzia hapo watu wote wakabaki midomo wazi!
Kwa mujibu wa mpasha habari za udaku huu rafiki wa "muheshimiwa" alikua katika pitapita zake za hapa na hale baada ya kumuona shemeji akizichapa kavu aliwasha simu yake na kurekodi video ya bure kisha akamtumia chifu video na kichwa cha habari "Una habari mkeo anazichapa ngumi kugombania bwana stendi?".    

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni