Alhamisi, 7 Januari 2016

SHEMEJI KWA SHEMEJI WAFUMANIANA LIVE!

Ilikua ni siku ya ijumaa nilipopokea simu kutoka kwa jamaa yangu wa Dar es Salaam kuwa bwana wikiendi hii tunakuja Mwanza na Fast Jet kula bata, kwakuwa nipo Wilayani Meatu nijitahidi wikiendi jioni tukutane Golden Crest pale Counter,nikamjibu hakuna shida.Nikajaza gari yangu mafuta full tank na kumpigia jamaa yangu mwingine aliye Shianyanga kwa jina anafahamika kama Alex kuwa asogee mpaka Mwigumbi ili tukutane njia panda kwa ajili ya kunipa kampani long drive kuelekea Mwanza.
Ilipofika saa moja usiku mimi na Alex tulikua tumeshafika Mwanza tukapata mahali pa kulala na kuamua kuanza kupata moja moto moja baridi katika ukumbi wa Villa Park uku tukijadili mambo ya hapa na pale kuhusu joto la uchaguziwa raisi na wabunge.Nikamjulisha jamaa yamgu wa kutoka Dar es Salaam kuwa nipo Villa Park na sio Golden Crest Hotel kwani  mida ilikua bado mapema.Yeye akanijibu kuwa muda si mrefu anakuja yupo na jamaa zake wawili aliombatana nao kutoka Dar es Salaam.
Mimi paoja na Alex tuliunganisha meza tatu pale karibu na counter na kuonezea viti na kufikia kama viti sita hivi.Punde si punde jamaaa yangu huyoo kwa jina anaitwa Gosbert ,na wenzake wawili wakatu join kwenye meza huku vinywaji vikiendelea kufurika mezani.Kumbuka kuwa huyu jamaa yangu wa Shinyanga hawa jamaa zangu wa Dar es Salaam hawafahamu na wao hawamfahamu kabisa.Baada ya kutambulishana wote tukaendelea kunywa uku mziki wa rhumba tukiusikia kwa karibu kabisa.Wadada wote waliokaaa karibu na meza yetu waliikodolea macho kwa tamaa ya kutaka kupata walau salamu tu kumbuka meza yetu tulikua tumekaa wanaume tu.Basi baada ya nusu saa jamaa mmoja kati ya wale walikuja kutoka Dar es Salaam John ambaye alikua ni bwana harusi kama mwaka mmoja umepita alimpungia mkono dada mmoja alikaa meza ya jirani kumpa ishara ya ukaribisho katika meza yetu iliyokua imefurika vinywaji vya kila aina.Dada alikua ameumbika kwa sura na shepu alikaribia meza yetu akakaa na kuendelea na mazungumzo ya kunong'onezana na mwenzetu aliyekua amemkaribisha.Baada ya saa moja hivi mwezetu alituomba radhi kuwa anaenda hotel kuna jambo akatafakari kidogo pamoja na huyo dada aliyemkaribisha mezani kwetu!
Tulimruhusu akatokomea gizani.Baadae kidogo kama dakika arobaini hivi walirudi tena mezani yeye na yule dada tukaendelea kutafuta kinywaji.
Huyu rafiki yangu wa Shinyanga,Alex ni mwanajeshi na amelelewa na baba yake mdogo kule Dar es Salaam na mwaka mmoja uliopita alienda kozi ya kijeshi hakuweza kuudhuria harusi ya mtoto wa mwisho wa baba yake mdogo aliyekua anaolewa na mume wa uyo dada yake hawafahamiani kwani tangu alipotoka kozi hawajaonana.
Baada ya kinywaji kuzidi kukolea ilibidi utambulisho uanze upya kama kawaida ya walevi wanavyokua sasa ikagundulika kuwa Alex na huyu jamaa aliyetoka na mchepuko ni mtu na shemeji yake yaani jamaa aliyetoka na mchepuko wife wake ndo yule dada aliyeolewa wakati Alex yupo kozi!
Ilibidi John azungushe tena raundi mbili mezani kama faini kwa ajili ya kufumaniwa na shemeji yake!

Maoni 1 :

  1. Huu ni lazima ushuhudia usomaji na kila mtu, nipo hapa kuruhusu ulimwengu wote kujua kuhusu mtu aliyeokoa uhusiano wangu na mtu huyu mkuu anaitwa Dr IZOYA. Hakika alifanya kazi nzuri kwangu kwa kumrudisha mpenzi wangu wa zamani ambaye aliniacha na kuahidi kamwe kurudi kwangu tena. Kwa hili, nimekuja kutambua kuwa kutoa maelezo ya Dk IZOYA kwa ulimwengu utafanya mengi mazuri kwa wale walio na nyumba zilizovunja au uhusiano kwa ajili yake ili kukusaidia kurekebisha uhusiano huo uliovunjika au ndoa yako. Unaweza kumfikia kupitia anwani yake ya barua pepe: drizayaomosolution@gmail.com au kumwita moja kwa moja kwenye [+12098373537]. Kuwasiliana naye na kuona jinsi tatizo lako litatatuliwa ndani ya 24hours. Pia mtaalamu katika mambo yafuatayo ...
    (1) Unataka kurudi nyuma yako.
    (2) Unataka kukuzwa katika ofisi yako.
    (3) Unataka wanaume / wanawake kukufuate.
    (4) Unataka mtoto.
    (5) Wewe ni mjasiriamali na unataka kushinda mikataba
    (6) Unataka mume wako awe wako milele
    (7) Unahitaji msaada wa kiroho.
    (8) Umeshambuliwa na unataka kupona fedha zilizopotea.
    (9) Weka talaka
    (10) Kualika kwa mila ya fedha
    (11) Chagua uchaguzi

    JibuFuta