Jumatano, 20 Januari 2016

KWA NINI WANAUME HUTOKA NJE?

Leo naomba tuchambue wote kwa pamoja kuhusu ni sababu gani zinazowafanya wanaume kutoka nje ya ndoa yaani "kuchepuka".Hizi sabau ni tofauti na zile zinazosababisha wanawake kutoka nje ya uhusiano ambazo tutaweza jadili siku zijazo:

Kuridhisha mwili kwanza:Kimaumbile inaelezwa kwamba mwanamume hahusishi tendo la ndoa na kupenda mtu.Kwa mwanaume  kupenda ni jambo jingine na la tendo la ndoa ni jamba lingine.Hii ni tofauti na wanawake ambao wanaonekana kuunganisha tendo la ndoa na kupenda,

Katika uhusiano wa kawaida wanawake huumia zaidi linapokuja suala la kusalitiana kwa sababu wao wanaposhiriki tendo la ndoa na mwanaume huwa wamempenda mwanaume huyo kutoka moyoni kabisa.
Lakini mwanaume anaweza kudai kwamba amempenda mwanamke na hata kufikia kumwoa au kumpa kila kitu ,wakati ukweli ni kwamba ,amevutiwa na mwili wake,anataka tu kufaidi mwili wake .Kwa mwanaume ,hivyo ni vitu viwili tofauti kupenda ni kitu kimoja na tendo la ndoa ni kitu kingine.

Ndio maana wanawake wanaojiuza mitaani usiku hupata soko kutoka kwa wanaume .Siyo kwamba wanaume wanaowachukua wanawake wale wamewapenda,hapana.Huwachukua ili kuridhisha tamaa zao za mwili.Ndiyo maana wakishamalizana,hawana kuuliza "kesho tutakutana wapi", kwasababu wamewapenda,HAPANA!Yule ameuza mwili wake na huyu amenunua mwili,hakuna kupendana.

Kuna wakati inatokea watu wanapokutana kwenye semina au kongamano na wakashawishika kugegedana na uhusiano huo ukaishia hapohapo na kusahaulika kila kitu hapohapo,hakuna kupendana kuna kutamani na kuonja,Waingereza wanaita "One Night Stand".

Kupenda kubadili mboga:
Hili linategemea na malezi na watu wanaomzunguka huyo mwanaume kwani wapo wanaume wanaoweza vumilia kuwa na uhusiano na mwanamke mmoja na wapo wanaume wanaoamini kuwa wao ni lazima wabadilishe wanawake tofauti tofauti kila  baada ya muda.Na wanafanya hivyo kwa sababu wanawake wapo na wanapatikana kiurahisi!
Ndiyo maana inadaiwa kwamba,wanaume wasiotoka nje ni wale ambao wana shughuli nyingi sana,wagonjwa au ambao hawana nafasi ya kuweza kutoka,vinginevyo ,kila mwanaume yuko kwenuye hatari ya kutoka na mwanamke hapaswi kumsemea mumwewe au mpenzi wake,kwamba hawezi kuchepuka.

Udadisi juu ya umbile la mwanamke:
Wanaume wana tabia ya kujiuliza maswali kuhusu aina fulani ya wanawake.Siyo tu suala la tamaa,bali ni suala la kutaka kujua zaidi kuhusu umbile fulani,kwa mfano makalio makubwa inakuaje au umbile la urefu sana kama twiga inakuaje kwney ukle "mtanange" wa sita kwa sita.Kwa kiasi fulani nao wanawake wana tatizo hilo lakini wanaume ni zaidi sana.Mwanaume kinachoenda mawazoni mwao ni kutaka kujua inavyokuwa kushiriki na mwanamke wa aina fulani,siyo kupenda ni kutaka kukata kiu ya udadisi wa kimwili.

Kupunguza hisa za kutojiamini na msongo wa mawazo:Mtu ambaye hajiamini anaweza kujaribu kujificha au kutafuta kujipandisha kupitia pombe,fedha magari ya kifahari na vitu vingine vya kifahari.Lakini pia anaweza kujihusisha na ngono za hovyo katika kujaribu katafuta nafuu yaani "relief".Baadhi ya wanaume kwa kutoka nje wanadhani wanahisi ahueni na kupanda kithamani.Kwa kadiri wanavyotoka nje ndivyo wanavyohisi penog na ndivyo wanavyozidi kutoka.Na hapa wanakua wanazidi kutengeneza tatizo la kisaikolojia katika nafsi zao.

Kutoridhishwa ndani:Mwanaume huchukulia kufanya mapenzi kama kitu kimoja na kupenda kama kitu kingine.Anapojikuta haridhishwi na mkewe huamua kwenda kutafuta ridhiko nje,anaweza kuwa bado anampenda mkewe,lakini mwili wake haujaridhishwa na kwa sababu kupenda kwa upande wake hakuna maana sawa na tendo la ndoa ,hutafuta mwili mwingine.

Kutojua kusudi la maisha:Hali hii huwakabili wanaume ambao wana fedha au hata umaarufu.Kwasababu walitafuta fedha au umaarufu bila ya kujua ni kwa sababu gani hasa na nini kinatakiwa kifuate baada ya kupata fedha au umaarufu ,huchanganyikiwa na kama akiwakatika mazingira ya kukutana na warembo basi kubadilisha wanawake inakua sehemu ya "life style" kwasababu hakujua itakuwa ivyo,na hakujiandaa kwa namna ya kuzikabili changamoto mbalimbali zinazosababishwa na iyo hadhi au "status" aliyopata muda huo.

Maoni 1 :

  1. Huu ni lazima ushuhudia usomaji na kila mtu, nipo hapa kuruhusu ulimwengu wote kujua kuhusu mtu aliyeokoa uhusiano wangu na mtu huyu mkuu anaitwa Dr IZOYA. Hakika alifanya kazi nzuri kwangu kwa kumrudisha mpenzi wangu wa zamani ambaye aliniacha na kuahidi kamwe kurudi kwangu tena. Kwa hili, nimekuja kutambua kuwa kutoa maelezo ya Dk IZOYA kwa ulimwengu utafanya mengi mazuri kwa wale walio na nyumba zilizovunja au uhusiano kwa ajili yake ili kukusaidia kurekebisha uhusiano huo uliovunjika au ndoa yako. Unaweza kumfikia kupitia anwani yake ya barua pepe: drizayaomosolution@gmail.com au kumwita moja kwa moja kwenye [+12098373537]. Kuwasiliana naye na kuona jinsi tatizo lako litatatuliwa ndani ya 24hours. Pia mtaalamu katika mambo yafuatayo ...
    (1) Unataka kurudi nyuma yako.
    (2) Unataka kukuzwa katika ofisi yako.
    (3) Unataka wanaume / wanawake kukufuate.
    (4) Unataka mtoto.
    (5) Wewe ni mjasiriamali na unataka kushinda mikataba
    (6) Unataka mume wako awe wako milele
    (7) Unahitaji msaada wa kiroho.
    (8) Umeshambuliwa na unataka kupona fedha zilizopotea.
    (9) Weka talaka
    (10) Kualika kwa mila ya fedha
    (11) Chagua uchaguzi

    JibuFuta