Jumanne, 5 Januari 2016

IVI NI KWELI NAIBIWA MKE WANGU?KERUUUUU!

Wadau muda si mrefu nimeingia hapa Ubungo River Side Bar kupata mupe mruke mupatie ili nipunguze makali ya foleni ya mataa ya Ubungo namkuta jamaa yangu macho yamemtoka kama vile kapata taarifa za msiba!Nilivuta kiti na kumsabahi hakuitikia,kwa gadhabu alikita meza kwa mkono na kuguna kwa kichaga,Keruuuu!
Nikamwambia kulikoni Chuwa kuna msiba?Akasema hapana ila wife wake kamfumania!
Nikamuuliza umemfumania wapi?Gesti au nyumbani?
Akasema hapana amefuma meseji kwenye simu yake alitumiwa na wife kimakosa.
Text ilisema ivi
"Sorry mi nilitaka tukae tu sehemu for story mambo fulani siko fit leo,lol pole!Nilikua kwa watu thus why sikutaka kukwambia kwa simu!"
Chuwa alivuta pumzi kwa nguvu uku akinikazima macho utadhani mimi ndo mgoni wake,
"Nashindwa kuelewa Meku maana huyu mlengwa sio mimi na sikuwa na chati nae!"
Niliagiza kinywaji cha Serenegti ya uvuguvugu nikiendelea kumsikiliza Chuwa kwa umakini nikaanza kumpa ushauri nasaha ili asije akasababisha madhara kwenye familia yake.
"Sikiliza Mangi,ingawa ni kweli sms inatia shaka lakini mkuu kubalia kuwa haipo "conclusive"
mfano je kama shem yupo na rafiki yake wa kike na wana mazoea ya kununuliana bia na kitimoto
alafu shem anatuma text "vipi wee bata umeshatoka kazini,mi nshatoka na sina ishu hapa home,tutoke kidogo,unaoonaje?"
Rafiki yake anajibu "poa wangu,mi nshatoka...vipi wataka twende kwa Swai?Upo njema?....maana leo ipo ya kukausha wangu,mi wallet tupu,na nilipokupigia mbona hukueleweka?"
Meku wife wako ndo akajibu"Sorry mi nilitaka tukae tu sehemu for story ,mambo flani siko fit leo lol pole!nilikuwa kwa watu thus why sikutaka kukwambia kwa simu".TATIZO LIPO WAPI JOMBAAA!Kunywa bia punguza hasira!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni