Jumatatu, 25 Januari 2016

TUFANYEJE BAADA YA FUMANIZI?

Kama ni mara ya kwanza unamfumania mpenzi wako au hata kama ni mara ya pili .lakini hukuwa unategemea kwamba,jambo hilo lingetokea tena,kwa kawaida,huwa kuna maumivu makali sana ya kihisia.Uamuzi unaoweza kuuchukuawakati huo unaweza usiwe wa busarasana.Kwa hiyo,baada ya fumanizi,inabidi utulie kwanza.Ni kweli kwamba utakuwa na mshtuko mkubwa ambao utakuumiza kihisia,ambapo,unaweza kukufanya uchukue uamuzi usio muafaka wakati mwingine katika hali ya kuchanganyikiwa.
Utulivu ni muhimu sana katika wakati huu wa mshtuko.Njia nzuri ya kupata utulivu ni kujitahidi kujiambia kwamba,huyo mpenzi wako mlikutana mkiwa watu wazima na kila mmoja akiwa na tabia na mienendo yake.Lakini ni kujitahidi kuwa mkweli kwa kutambua kwamba,binadamu ni dhaifu.Uamuzi wa ufanye nini unatakiwa utolewe baada ya kipindi cha mshtuko kupita.Hapa lazima ujiulize kama ni kweli mtaweza kuishi vizuri baada ya tukio hilo,hasa kwa kuzingatia hali ya uhusiano wenu kwa ujumla hata kabla ya kufumaniwa.
Mwanamke mmoja ambaye alimfumania mumewe akiwa anafanya mapenzi na binti aliyekuwa akiuza duka lao la maua,aliwahi kuniambia kwamba,kuna wakati inakuwa vigumu."Mimi nilikua naamua kwamba .ninaondoka ,siweiz,lakini baadaye najiambia ngoja nikae tu.Baadaye tena nabadili mawazo,nasema naondoka"!
Ni kweli hii huweza tokea ila unachotakiwa kufanya ni usikubali uongozwe na hisia, bali uongozwe na nafsi.Isikilize nafsi yako zaidi kuliko hisia.
Ni hatari sana kwa kipindi hiki kama kuwasikiliza ndugu au marafiki,wazazi au watu wengine ambao tunaamini kwamba ,wanaweza kutusaidia kimawazo.

Inabidi mfumaniaji akae chini na mfumaniwaji na kuangalia kama anadhani kuna haja ya kuendelea kuishi pamoja baada ya tukio hilo na amuulize anavyohisi yeye (mfumaniwaji)  ua aangalie namna mfumaniwaji alivyolichukulia hilo tukio.
Ila kuuliza kwa upendo baada ya tukio husaidia sana mtu kujua ukweli.
Kuna wafumaniwaji ambao huwa wanasema  wanachofikiria.Kama wanaona hawana haja tena na wapenzi wao husema ukweli na kama wanaamini bado wanawahitaji,husema hivyo na nia na dhati ya maneno yao huweza kupimika kirahisi.  

Maoni 1 :

  1. Huu ni lazima ushuhudia usomaji na kila mtu, nipo hapa kuruhusu ulimwengu wote kujua kuhusu mtu aliyeokoa uhusiano wangu na mtu huyu mkuu anaitwa Dr IZOYA. Hakika alifanya kazi nzuri kwangu kwa kumrudisha mpenzi wangu wa zamani ambaye aliniacha na kuahidi kamwe kurudi kwangu tena. Kwa hili, nimekuja kutambua kuwa kutoa maelezo ya Dk IZOYA kwa ulimwengu utafanya mengi mazuri kwa wale walio na nyumba zilizovunja au uhusiano kwa ajili yake ili kukusaidia kurekebisha uhusiano huo uliovunjika au ndoa yako. Unaweza kumfikia kupitia anwani yake ya barua pepe: drizayaomosolution@gmail.com au kumwita moja kwa moja kwenye [+12098373537]. Kuwasiliana naye na kuona jinsi tatizo lako litatatuliwa ndani ya 24hours. Pia mtaalamu katika mambo yafuatayo ...
    (1) Unataka kurudi nyuma yako.
    (2) Unataka kukuzwa katika ofisi yako.
    (3) Unataka wanaume / wanawake kukufuate.
    (4) Unataka mtoto.
    (5) Wewe ni mjasiriamali na unataka kushinda mikataba
    (6) Unataka mume wako awe wako milele
    (7) Unahitaji msaada wa kiroho.
    (8) Umeshambuliwa na unataka kupona fedha zilizopotea.
    (9) Weka talaka
    (10) Kualika kwa mila ya fedha
    (11) Chagua uchaguzi

    JibuFuta