Jumapili, 31 Januari 2016

WANAWAKE MNALIJUA HILI?

Kwa sababu mbalimbali ,mwanamume anaweza kuhisi kwamba,mkewe hampi heshima yake kutokana na matatizo yake mbalimbali.Kwa mfano mume ameanguka kimapato,mwanamke anapoonesha kwamba hajaridhishwa na jambo hilo kiasi kwamba,inaonekana kama anamlaumu mumewe,uwezekano wa mume huyo kutoka ni mkubwa.
  Anatoka kwa sababu anataka kwenda kuthibitisha huko nje kwamba,bado anamudu ,ana nguvu na uwezo,tofauti na mkewe anavyofikiria.Mara nyingi huenda kuchukua wasichana wadogo sana ukilinganisha na mkewe.Kuchukua huku wasichana wadogo sana ni nia yake(bila mwenyewe kujua) kujithibitishia kwamba,anayo thamani, kwani anapendwa na wasichana wadogo.Hivyo ndivyo inavyokua.Kuna mtu aliwahi kuniambia kwamba ,mkewe anamdharau kwasababu ati hajamudu kufanya mambo ya maendeleo kama wenzake ofisini kwake.Alinambia kwamba,hajali jinsi mkewe anavyomdharau kwa sababu kuna wasichana wabichi na warembo ambao wanamheshimu na kumpenda kikweli!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni