Jumatano, 6 Januari 2016

WIFE BAADA YA KUUFAHAMU MCHEPUKO KANIPA BIG UP

Chrismass ya mwaka uliopita kwangu ilikua balaa sikusherehekea vizuri kutokana na kukutwa na kimeo ndani.Ilikua hivi yaani mkesha wote wa Krissmass niliishia usiku mzima kumbembeleza wife anisamehe kutokana na kusoma meseji za malavidavi toka kwa mchepuko wangu.
Alilia sana ghafla akanyamaza akaniuliza nakosa nini kwake,nikamjibu hakuna,
akaniuliza tena huo mchepuko unakitu gani au kivipi kumzidi yeye mpaka nimsaliti,asije akawa analia kumbe mchepuko wenyewe unasura ngumu alafu mbaya tu!
Nikamjibu ni wa kawaida tu ,ila moyoni najua ni mkali kumzidi yeye!
Akaniambia nikitaka suluhu basi auone na niuambie mbele yake kwamba its over between mimi na yeye(mchepuko).
Nilibisha bisha at last kwasababu nampenda kikweli kweli my wife nikaona isiwe tabau ngojea niokoe ndoa yangu na familia yangu.Simu yangu ikaendelea kushikiliwa na wife.
Jana asubuhi nikaupigia simu chini ya uangalizi wa wife on loud speaker nikauomba tuonane pale maeneo ya Villa Park Mwanza mida ya saa kumi na mbili kabla band haijaazna kupiga mziki.Ilipofika saa kumi na moja na nusu mimi na wife tulikua tumeshafika eneo la tukio,niliagiza bia kwa kujikaza kiume tu lakini kooni ilikwama kwani sikuwa na hamu nayo nilikua nawaza reaction za wife dhidi ya mchepuko itakuaje?
Nikiwa kwenye dimbwi zito la mawazo mara mlengwa huyo aliingia getini na kuanza kuangaza macho,wife ndo alikua wa kwanza kumuona akauliza ndio huyo?Nikamjibu kwa kichwa tu huku mapigo ya moyo yakiongezeka na kujisikia tumbo la kuhara,mate mdomoni yalikauka!
Mchepuko ukiwa umejikwetua na mini  skirt yake alijivuta moja kwa moja upande niliokua nimekaa huku akisindikizwa na macho ya watu wengi nadhani kwa anayepafahamu Villa Park palivyo atakubaliana na mimi,alifika kwangu uku akiwa na smile kubwa usoni ata mimi sikutaka kumwangalia usoni.
Kifupi ni mzuri kwa sura  na umbile lake ni shida!tako kubwa ukichanganya na miondoko akipita barabarani watu wazima lazima wageuke, yaani ni changamoto!
Nikajua leo nimekwisha.Cha kushangaza wife akanipa ishara kuwa anainuka nimsalimie mchepuko then nimfuatye pale kwenye gari.(wife alikua amekaa meza ya jirani kunichora).
Nikabaki nimepigwa na butwaa na uamuzi wa wife nikajikaza kisabuni nika upa hug bubu nikamwita muhudumu amletee Saint Anna,nilimwomba akae nakuja,then nikamfuata wife.
Kufika nakuta kwenye gari wife amekaa juu ya boneti ana smile,akaniambia weeeeew mshenzi malaya mkubwa unajua kweli kuopoa,ulimpata wapi huyu?
Kabla sijajibu akanimbia alisoma nae chuo na enzi hizo alikua miongoni mwa mademu watano wakali chuoni (top five hotiest gals).
Kwa kunishangaza zaidi akaniambia una bahati nimemkubali ingia kwenye gari tuondoke!

Akachukua simu yangu akampiga mchepuko akimwambia asinitafute tena!
Usiku wa kuamkia leo nilikua honey moon nimepewa mahaba na wife yaani first grade!haijapata kutokea!Hahahaaaa hatare!

Maoni 1 :

  1. Huu ni lazima ushuhudia usomaji na kila mtu, nipo hapa kuruhusu ulimwengu wote kujua kuhusu mtu aliyeokoa uhusiano wangu na mtu huyu mkuu anaitwa Dr IZOYA. Hakika alifanya kazi nzuri kwangu kwa kumrudisha mpenzi wangu wa zamani ambaye aliniacha na kuahidi kamwe kurudi kwangu tena. Kwa hili, nimekuja kutambua kuwa kutoa maelezo ya Dk IZOYA kwa ulimwengu utafanya mengi mazuri kwa wale walio na nyumba zilizovunja au uhusiano kwa ajili yake ili kukusaidia kurekebisha uhusiano huo uliovunjika au ndoa yako. Unaweza kumfikia kupitia anwani yake ya barua pepe: drizayaomosolution@gmail.com au kumwita moja kwa moja kwenye [+12098373537]. Kuwasiliana naye na kuona jinsi tatizo lako litatatuliwa ndani ya 24hours. Pia mtaalamu katika mambo yafuatayo ...
    (1) Unataka kurudi nyuma yako.
    (2) Unataka kukuzwa katika ofisi yako.
    (3) Unataka wanaume / wanawake kukufuate.
    (4) Unataka mtoto.
    (5) Wewe ni mjasiriamali na unataka kushinda mikataba
    (6) Unataka mume wako awe wako milele
    (7) Unahitaji msaada wa kiroho.
    (8) Umeshambuliwa na unataka kupona fedha zilizopotea.
    (9) Weka talaka
    (10) Kualika kwa mila ya fedha
    (11) Chagua uchaguzi

    JibuFuta